Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Maombi
1 Wafalme 18 : 39
39 Na watu wote walipoona, wakaanguka kifudifudi; wakasema, BWANA ndiye Mungu, BWANA ndiye Mungu.
Zaburi 5 : 3
3 BWANA, asubuhi utaisikia sauti yangu, Asubuhi nitakupangia dua yangu na kutazamia.
Zaburi 88 : 13
13 Lakini mimi nimekulilia Wewe, BWANA, Na asubuhi maombi yangu yatakuwasilia.
Zaburi 143 : 8
8 Uniwezeshe kusikia fadhili zako asubuhi, Kwa maana nimekutumaini Wewe. Unifundishe njia nitakayoiendea, Kwa maana ninakuinulia nafsi yangu.
Isaya 33 : 2
2 Ee BWANA, uturehemu; tumekungoja wewe; uwe wewe mkono wetu[7] kila asububi, na wokovu wetu pia wakati wa taabu.
Zaburi 88 : 1
1 Ee BWANA, Mungu wa wokovu wangu Mchana na usiku nimelia mbele zako.
Zaburi 55 : 17
17 Jioni, asubuhi, na adhuhuri nitalalama na kuugua, Naye ataisikia sauti yangu.
Danieli 6 : 10
10 Hata Danieli, alipojua ya kuwa yale maandiko yamekwisha kutiwa sahihi, akaingia nyumbani mwake, (na madirisha katika chumba chake yalikuwa yamefunguliwa kuelekea Yerusalemu;) akapiga magoti mara tatu kila siku, akasali, akashukuru mbele za Mungu wake, kama alivyokuwa akifanya tokea hapo.
Luka 6 : 12
12 ⑳ Ikawa siku zile aliondoka akaenda mlimani ili kuomba, akakesha usiku kucha akimwomba Mungu.
1 Wathesalonike 5 : 17
17 ombeni bila kukoma;
Waraka kwa Waebrania 4 : 16
16 Basi na tukikaribie kiti cha neema kwa ujasiri, ili tupewe rehema, na kupata neema ya kutusaidia wakati wa mahitaji.
Mwanzo 18 : 32
32 ③ Akasema, Bwana asiwe na hasira, nami nitasema mara hii tu, Huenda wakaonekana huko kumi? Akasema, Sitaharibu kwa ajili ya hao kumi.
Kutoka 33 : 12
12 Musa akamwambia BWANA, Angalia, wewe waniambia, Wachukue watu hawa; nawe hukunijulisha ni nani utakayemtuma pamoja nami. Lakini umesema, Nakujua jina lako, nawe umepata neema mbele zangu.
Kutoka 33 : 18
18 ② Akasema, Nakusihi unioneshe utukufu wako.
Mwanzo 24 : 63
63 ⑦ Isaka akatoka ili kutafakari shambani wakati wa jioni; akainua macho yake, akaona, kuna ngamia wanakuja.
Mathayo 6 : 6
6 Bali wewe usalipo, ingia katika chumba chako cha ndani, na ukiisha kufunga mlango wako, usali mbele za Baba yako aliye sirini; na Baba yako aonaye sirini atakujazi.
Zaburi 5 : 1 – 168
1 Ee BWANA, uyasikilize maneno yangu, Ukuangalie kutafakari kwangu.
2 Uisikie sauti ya kilio changu, Ee Mfalme wangu na Mungu wangu, Kwa maana Wewe ndiwe nikuombaye.
3 BWANA, asubuhi utaisikia sauti yangu, Asubuhi nitakupangia dua yangu na kutazamia.
4 Maana huwi Mungu apendezwaye na ubaya; Mtu mwovu hatakaa kwako;
5 Wajivunao hawatasimama mbele za macho yako; Unawachukia wote watendao uovu.
6 Utawaharibu wasemao uongo; BWANA humchukia mwuaji na mwenye hila
7 Bali mimi, kwa wingi wa fadhili zako, Nitaingia nyumbani mwako; Na kusujudu kwa kicho, Nikilielekea hekalu lako takatifu.
8 BWANA, uniongoze kwa haki yako, Kwa sababu yao wanaoniotea. Uinyoshe njia yako mbele ya uso wangu,
9 Maana vinywani mwao hamna uaminifu; Moyo wao ni shimo tupu, koo lao ni kaburi wazi, Ulimi wao hujipendekeza.
10 Wewe, Mungu, uwapatilize, Na waanguke kwa mashauri yao. Uwatoe nje kwa ajili ya wingi wa makosa yao, Kwa maana wamekuasi Wewe.
11 ① Nao wote wanaokukimbilia watafurahi; Watapiga kelele za furaha daima. Kwa kuwa Wewe unawahifadhi, Walipendao jina lako watakufurahia.
12 Kwa maana Wewe utambariki mwenye haki; BWANA, utamzungushia radhi kama ngao.
Leave a Reply