Biblia inasema nini kuhusu Maombezi – Mistari yote ya Biblia kuhusu Maombezi

Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Maombezi

1 Samweli 2 : 25
25 ⑦ Mtu mmoja akimkosea mwenzake, Mungu atamhukumu; lakini mtu akimkosea BWANA, ni nani atakayemtetea? Lakini hawakuisikia sauti ya baba yao, kwa sababu BWANA amekusudia kuwaua.

Mwanzo 37 : 22
22 Reubeni akawaambia, Msimwage damu; mtupeni katika shimo hili lililopo nyikani, wala msimguse; ili apate kumwokoa katika mikono yao, akamrudishe kwa baba yake.

Mwanzo 37 : 27
27 ⑪ Haya, na tumuuze kwa hawa Waishmaeli, wala mikono yetu isimdhuru, maana yeye ni ndugu yetu, na damu yetu. Ndugu zake wakakubali.

Mwanzo 41 : 13
13 Ikawa, kama vile alivyotufasiria ndivyo ilivyotokea; mimi nilirudishwa katika kazi yangu, na yeye alitundikwa.

Mwanzo 40 : 14
14 ⑯ Ila unikumbuke mimi, utakapopata mema, ukanifanyie fadhili, nakuomba, ukanitaje kwa Farao, na kunitoa katika nyumba hii.

1 Samweli 19 : 7
7 Basi Yonathani akamwita Daudi, naye Yonathani akamjulisha mambo hayo yote. Kisha Yonathani akamleta Daudi kwa Sauli, naye alikuwa akihudumu mbele yake, kama hapo awali.

1 Samweli 25 : 35
35 ⑫ Basi Daudi akapokea mkononi mwake vitu vile alivyomletea; akamwambia, Haya! Kwea kwa amani kwenda nyumbani kwako; tazama, nimeisikiliza sauti yako, nami nimelikubali ombi lako.

2 Samweli 14 : 24
24 Naye mfalme akasema, Ageukie nyumbani kwake, asinione uso wangu. Basi Absalomu akarejea nyumbani kwake, asimwone uso mfalme.

1 Wafalme 1 : 31
31 Ndipo Bathsheba akainama kifudifudi, akamsujudia mfalme, akasema, Bwana wangu mfalme Daudi na aishi milele.

1 Wafalme 2 : 25
25 Mfalme Sulemani akatuma kuwa jambo hilo liwe mkononi mwa Benaya mwana wa Yehoyada: naye akampiga, hata akafa.

2 Wafalme 4 : 13
13 Akamwambia, Sema naye sasa, Tazama, wewe umetutunza sana namna hii; utendewe nini basi? Je! Uombewe neno kwa mfalme, au kwa kamanda wa jeshi? Yule mwanamke akamjibu, Mimi ninakaa katika watu wangu mwenyewe.

2 Wafalme 5 : 8
8 ③ Ikawa, Elisha, yule mtu wa Mungu, aliposikia kwamba mfalme wa Israeli ameyararua mavazi yake, ndipo akatuma mtu kwa mfalme, akisema, Mbona umeyararua mavazi yako? Na aje sasa kwangu mimi, naye atajua ya kuwa yuko nabii katika Israeli.

Filemoni 1 : 21
21 Kwa kuwa nakuamini kutii kwako ndiyo maana nimekuandikia, nikijua ya kuwa utafanya zaidi ya hayo nisemayo.

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *