Biblia inasema nini kuhusu mambo mabaya yanayowapata watu wema – Mistari yote ya Biblia kuhusu mambo mabaya yanayowapata watu wema

Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia mambo mabaya yanayowapata watu wema

Yohana 9 : 1 – 41
1 ③ Na alipokuwa akipita alimwona mtu, kipofu tangu kuzaliwa.
2 ④ Wanafunzi wake wakamwuliza wakisema, Rabi, ni yupi aliyetenda dhambi, mtu huyu au wazazi wake, hata azaliwe kipofu?
3 ⑤ Yesu akajibu, Huyu hakutenda dhambi, wala wazazi wake; bali kazi za Mungu zidhihirishwe ndani yake.
4 ⑥ Imetupasa kuzifanya kazi zake yeye aliyenituma maadamu ni mchana, usiku waja asipoweza mtu kufanya kazi.
5 ⑦ Muda nilipo ulimwenguni, mimi ni nuru ya ulimwengu.
6 ⑧ Alipokwisha kusema hayo, alitema mate chini, akafanya tope kwa yale mate. Akampaka kipofu tope machoni,
7 akamwambia, Nenda ukanawe katika bwawa la Siloamu, (maana yake, Aliyetumwa). Basi akaenda na kunawa; akarudi akiwa anaona.
8 Basi jirani zake, na wale waliomwona zamani kuwa ni mwombaji, wakasema, Je! Huyu siye yule aliyekuwa akiketi na kuomba?
9 Wengine wakasema, Ndiye. Wengine wakasema, La, lakini amefanana naye. Yeye mwenyewe alisema, Mimi ndiye.
10 Basi wakamwambia, Macho yako yalifumbuliwaje?
11 Yeye akajibu, Mtu yule aitwaye Yesu alifanya tope, akanipaka macho akaniambia, Nenda Siloamu ukanawe; basi nikaenda na kunawa, nikapata kuona.
12 Wakamwambia, Yuko wapi huyo? Akasema, Mimi sijui.
13 Basi wakampeleka kwa Mafarisayo yule aliyekuwa kipofu zamani.
14 ⑩ Nayo ilikuwa sabato, hapo Yesu alipofanya zile tope na kumfumbua macho.
15 Basi Mafarisayo nao wakamwuliza tena jinsi gani alivyopata kuona. Akawaambia, Alinitia tope juu ya macho, nami nikanawa, na sasa naona.
16 ⑪ Basi baadhi ya Mafarisayo wakasema, Mtu huyo hakutoka kwa Mungu, kwa sababu haishiki sabato. Wengine wakasema, Awezaje mtu mwenye dhambi kufanya ishara kama hizo? Kukawa na utengano kati yao.
17 ⑫ Basi wakamwambia yule kipofu mara ya pili, Wewe wasemaje kuhusu habari zake kwa vile alivyokufumbua macho? Akasema, Ni nabii.
18 Basi Wayahudi hawakuamini habari zake, ya kuwa alikuwa kipofu, kisha akapata kuona; hadi walipowaita wazazi wake yule aliyepata kuona.
19 Wakawauliza wakisema, Huyu ndiye mwana wenu, ambaye mnasema kwamba alizaliwa kipofu? Amepataje, basi, kuona sasa?
20 Wazazi wake wakawajibu, wakasema, Tunajua ya kuwa huyu ndiye mwana wetu, tena ya kuwa alizaliwa kipofu;
21 lakini jinsi aonavyo sasa hatujui; wala hatujui ni nani aliyemfumbua macho. Mwulizeni yeye mwenyewe; yeye ni mtu mzima; atajisemea mwenyewe.
22 ⑬ Wazazi wake waliyasema hayo kwa sababu waliwaogopa Wayahudi; kwa maana Wayahudi walikuwa wamekwisha kukubaliana kwamba mtu akimkiri kuwa ni Kristo, atatengwa na sinagogi.
23 Ndiyo sababu wale wazazi wake walisema, Ni mtu mzima, mwulizeni yeye.
24 ⑭ Basi mara ya pili wakamwita yule mtu aliyekuwa kipofu, wakamwambia, Mpe Mungu utukufu. Sisi tunajua ya kuwa mtu huyo ni mwenye dhambi.
25 Basi yule mtu akajibu, Kwamba yeye ni mwenye dhambi sijui. Najua neno moja, kuwa mimi nilikuwa kipofu na sasa naona.
26 Basi wakamwambia, Alikutendea nini? Alikufumbua macho jinsi gani?
27 Akawajibu, Nimekwisha kuwaambia, wala hamkusikia; mbona mnataka kusikia tena? Ninyi nanyi mnataka kuwa wanafunzi wake?
28 Basi wakamshutumu, wakasema, Wewe u mwanafunzi wake yule; sisi tu wanafunzi wa Musa.
29 Sisi tunajua ya kuwa Mungu alisema na Musa; bali yule hatujui atokako.
30 Yule mtu akajibu, akawaambia, Hii ni ajabu! Kwamba ninyi hamjui atokako, naye alinifumbua macho!
31 ⑮ Tunajua ya kuwa Mungu hawasikii wenye dhambi; bali mtu akiwa ni mcha Mungu, na kuyafanya mapenzi yake, humsikia huyo.
32 Tokea hapo haijasikiwa ya kuwa mtu ameyafumbua macho ya mtu, ambaye alizaliwa kipofu.
33 ⑯ Kama huyo asingalitoka kwa Mungu, asingeweza kutenda neno lolote.
34 ⑰ Wakajibu, wakamwambia, Ama! Wewe ulizaliwa katika dhambi tupu, nawe unatufundisha sisi? Wakamtoa nje.
35 Yesu akasikia kwamba wamemtoa nje; naye alipomwona alisema, Wewe wamwamini Mwana wa Mungu?
36 Naye akajibu akasema, Ni nani, Bwana, nipate kumwamini?
37 ⑱ Yesu akamwambia, Umemwona, naye anayesema nawe ndiye.
38 Akasema, Naamini, Bwana. Akamsujudia.
39 ⑲ Yesu akasema, Mimi nimekuja ulimwenguni humu kwa hukumu, ili wao wasioona waone, nao wanaoona wawe vipofu.
40 ⑳ Baadhi ya Mafarisayo waliokuwapo pamoja naye wakasikia hayo, wakamwambia, Je! Sisi nasi tu vipofu?
41 Yesu akawaambia, Kama mngekuwa vipofu, msingekuwa na dhambi; lakini kwa kuwa sasa mwasema, Twaona; basi dhambi yenu inakaa.

Warumi 8 : 28
28 Nasi twajua ya kuwa katika mambo yote Mungu hufanya kazi pamoja na wale wampendao katika kuwapatia mema, yaani, wale walioitwa kwa kusudi lake.

Yeremia 29 : 11
11 Maana nayajua mawazo ninayowawazia ninyi, asema BWANA, ni mawazo ya amani wala si ya mabaya, kuwapa ninyi tumaini siku zenu za baadaye.

Ufunuo 21 : 4
4 ② Naye atafuta kila chozi katika macho yao, wala mauti haitakuwapo tena; wala maombolezo, wala kilio, wala maumivu hayatakuwapo tena; kwa kuwa mambo ya kwanza yamekwisha kupita.

1 Wakorintho 13 : 12
12 Maana sasa tunaona kwa kioo kwa jinsi ya fumbo; wakati ule tutaona uso kwa uso; sasa nafahamu kwa sehemu; wakati ule nitajua sana kama mimi nami ninavyojuliwa sana.

Zaburi 10 : 1 – 18
1 Ee BWANA, kwa nini wasimama mbali? Kwani unajificha nyakati za shida?
2 Kwa kiburi chake asiye haki mnyonge anafuatiwa kwa ukali; Na wanaswe kwa hila zizo hizo walizoziwaza.
3 Maana mdhalimu hujisifia tamaa ya nafsi yake, Na mwenye choyo humkana BWANA na kumdharau.
4 Mdhalimu kwa kiburi cha uso wake Asema, Mungu Hatapatiliza. Mawazo yake yote ni, Hakuna Mungu;
5 Njia zake ni thabiti kila wakati. Hukumu zako ziko juu asizione, Adui zake wote awakaripia.
6 Asema moyoni mwake, Sitaondoshwa, Kizazi baada ya kizazi sitakuwamo taabuni.
7 Kinywa chake kimejaa laana, Na hila na dhuluma. Chini ya ulimi wake kuna madhara na uovu,
8 Hujificha na kuotea vijijini. Katika maficho humwua asiye na hatia, Macho yake humtazama kisiri mtu duni.
9 Huotea faraghani kama simba pangoni, Huotea amkamate mtu mnyonge. Naam, humkamata mtu mnyonge, Na kumkokota akiwa wavuni mwake.
10 Hujikunyata na kuinama; Watu duni huanguka kwa nguvu zake.
11 Asema moyoni mwake, Mungu amesahau, Auficha uso wake, haoni kamwe.
12 Inuka, Ee Mungu BWANA, uuinue mkono wako, Ee Mungu Usiwasahau wanyonge.
13 Kwa nini mdhalimu amdharau Mungu. Akisema moyoni mwake, Hutapatiliza?
14 Umeona, maana unaangalia matatizo na dhiki, Uyatwae mkononi mwako. Mtu duni hukuachia nafsi yake, Maana umekuwa msaidizi wa yatima.
15 Uuvunje mkono wa mdhalimu, Na mwovu, uipatilize dhuluma yake, hadi usiione.
16 BWANA ndiye Mfalme milele na milele; Mataifa yataangamia kutoka nchi yake.
17 BWANA, utayasikia matakwa ya wanyonge, Uutaidhibiti mioyo yao, utalitega sikio lako.
18 Ili kumhukumu yatima na aliyeonewa, Binadamu aliye udongo asizidi kudhulumu.

Mathayo 5 : 45
45 ili mpate kuwa wana wa Baba yenu aliye mbinguni; maana yeye huwaangazia jua lake waovu na wema, huwanyeshea mvua wenye haki na wasio haki.

Zaburi 13 : 1 – 6
1 Ee BWANA, utanisahau hadi lini, hata milele? Hadi lini utanificha uso wako?
2 Nitakuwa na wasiwasi rohoni mwangu hadi lini, Nikihuzunika moyoni mchana kutwa? Adui yangu atatukuka juu yangu hadi lini?
3 Ee BWANA, Mungu wangu, uangalie, uniitikie; Uyatie nuru macho yangu, Nisije nikalala usingizi wa mauti.
4 Adui yangu asije akasema, Nimemshinda; Watesi wangu wasifurahi ninapoondoshwa.
5 Lakini mimi nimezitumainia fadhili zako; Moyo wangu na uufurahie wokovu wako.
6 Naam, nitamwimbia BWANA, Kwa kuwa amenitendea kwa ukarimu.

1 Yohana 2 : 15
15 Msiipende dunia, wala mambo yaliyomo katika dunia. Mtu akiipenda dunia, kumpenda Baba hakumo ndani yake.

Mathayo 13 : 18 – 23
18 Basi ninyi sikilizeni mfano wa mpanzi.
19 Kila mtu alisikiapo neno la ufalme bila kulielewa, huja yule mwovu, akalinyakua lililopandwa moyoni mwake. Huyo ndiye aliyepandwa karibu na njia.
20 Naye aliyepandwa penye miamba, huyo ndiye alisikiaye lile neno, akalipokea mara kwa furaha;
21 lakini hana mizizi ndani yake, bali hudumu kwa muda; ikitukia dhiki au udhia kwa ajili ya lile neno, mara huchukizwa.
22 Naye aliyepandwa penye miiba, huyo ndiye alisikiaye lile neno; na shughuli za dunia, na udanganyifu wa mali hulisonga lile neno; likawa halizai.
23 Naye aliyepandwa penye udongo mzuri, huyo ndiye alisikiaye lile neno, na kulielewa; yeye ndiye azaaye matunda, huyu mia, na huyu sitini, na huyu thelathini.

1 Wakorintho 11 : 29 – 30
29 Maana alaye na kunywa, hula na kunywa hukumu ya nafsi yake, kwa kutokuupambanua ule mwili.
30 ⑳ Kwa sababu hiyo wako wengi kwenu walio wagonjwa na dhaifu, na watu kadhaa wamelala.

Isaya 57 : 1
1 Mwenye haki hupotea, wala hakuna atiaye hayo moyoni; na watu watauwa huondolewa, wala hakuna afikiriye ya kuwa mwenye haki ameondolewa asipatikane na mabaya.

Luka 13 : 2 – 3
2 Akawajibu akawaambia, Je! Mwadhani ya kwamba Wagalilaya hao walikuwa wenye dhambi kuliko Wagalilaya wote, hata wakapatwa na mambo hayo?
3 Nawaambia, Sivyo; lakini msipotubu, ninyi nyote mtaangamia vivyo hivyo.

Ayubu 14 : 1
1 Mwanadamu aliyezaliwa na mwanamke Siku zake za kuishi si nyingi, naye hujaa taabu.

1 Wakorintho 10 : 13
13 Jaribu halikuwapata ninyi, isipokuwa lililo kawaida ya wanadamu; ila Mungu ni mwaminifu; ambaye hatawaacha mjaribiwe kupita muwezavyo; lakini pamoja na lile jaribu atafanya na mlango wa kutokea, ili muweze kustahimili.

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *