Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia malezi ya watoto
Zaburi 82 : 3 – 4
3 Mfanyieni hukumu maskini na yatima; Mtendeeni haki aliyeonewa, na fukara;
4 Mwokoeni maskini na mhitaji; Mwopoeni mikononi mwa wadhalimu.
Marko 9 : 37
37 Mtu akimpokea mtoto mmoja wa namna hii kwa jina langu, anipokea mimi; na mtu akinipokea mimi, humpokea, si mimi, bali yeye aliyenituma.
Zaburi 72 : 4
4 Na atawatetea watu walioonewa, Awaokoe wahitaji, na kumwaangamiza mdhalimu.
2 Wakorintho 9 : 6 – 8
6 Lakini nasema neno hili, Apandaye haba atavuna haba; apandaye kwa ukarimu atavuna kwa ukarimu.
7 Kila mtu na atende kama alivyokusudia moyoni mwake, si kwa huzuni, wala si kwa lazima; maana Mungu humpenda yeye atoaye kwa moyo mkunjufu.
8 Na Mungu aweza kuwajaza kila neema kwa wingi, ili ninyi, mkiwa na riziki za kila namna siku zote, mpate kuzidi sana katika kila tendo jema;
Mathayo 18 : 5
5 Na yeyote atakayempokea mtoto mmoja mfano wa huyu kwa jina langu, anipokea mimi;
Zaburi 10 : 14
14 Umeona, maana unaangalia matatizo na dhiki, Uyatwae mkononi mwako. Mtu duni hukuachia nafsi yake, Maana umekuwa msaidizi wa yatima.
Marko 10 : 14
14 Ila Yesu alipoona alichukizwa sana, akawaambia, Waacheni watoto wadogo waje kwangu, msiwazuie; kwa maana watoto kama hawa ufalme wa Mungu ni wao.
Yakobo 1 : 27
27 Dini iliyo safi, isiyo na dosari mbele za Mungu Baba ni hii, Kwenda kuwatazama yatima na wajane katika dhiki yao, na kujilinda na dunia pasipo mawaa.
1 Samweli 1 : 27
27 Niliomba nipewe mtoto huyu; BWANA akanipa dua yangu niliyomwomba;
Zaburi 72 : 13 – 14
13 Atawahurumia wanyonge na maskini, Na nafsi za wahitaji ataziokoa.
14 Atawakomboa kutoka kwa maonevu na udhalimu, Maana damu yao ina thamani machoni pake.
Mathayo 25 : 40
40 Na Mfalme atajibu, akiwaambia, Amin, nawaambia, kadiri mlivyomtendea mmojawapo wa hao ndugu zangu walio wadogo, mlinitendea mimi.
Isaya 1 : 17
17 jifunzeni kutenda mema; takeni hukumu na haki; wasaidieni walioonewa; mpatieni yatima haki yake; mteteeni mjane.
Yohana 13 : 34
34 Amri mpya nawapa, Mpendane. Kama vile nilivyowapenda ninyi, nanyi mpendane vivyo hivyo.
Mambo ya Walawi 19 : 33
33 Na mgeni akikaa pamoja nawe katika nchi yako, usimdhulumu.
Leave a Reply