Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Majaribu
Mwanzo 3 : 13
13 ⑯ BWANA Mungu akamwambia mwanamke, Nini hili ulilolifanya? Mwanamke akasema, Nyoka alinidanganya, nikala.
Mwanzo 20 : 6
6 Mungu akamwambia katika ndoto, Nami nimejua ya kwamba kwa ukamilifu wa moyo wako umefanya hivi, ndipo nami nikakuzuia usinitendee dhambi, kwa hiyo sikukuacha umguse.
Kutoka 34 : 16
16 ⑱ Ukawaoza wana wako binti zao, nao binti zao wakaenda kufanya uzinzi na miungu yao, wakawavuta wana wenu wafanye uzinzi na miungu yao.
Kumbukumbu la Torati 7 : 25
25 ⑥ Sanamu za kuchonga za miungu yao mtaziteketeza kwa moto; usitamani fedha wala dhahabu iliyo juu yao, wala usiitwae iwe yako usije ukanaswa nayo; kwa maana ni machukizo kwa BWANA, Mungu wako;
Kumbukumbu la Torati 8 : 14
14 ⑯ basi hapo moyo wako usiinuke, ukamsahau BWANA, Mungu wako, aliyekutoa katika nchi ya Misri, katika nyumba ya utumwa;
Kumbukumbu la Torati 8 : 18
18 ⑳ Bali utamkumbuka BWANA, Mungu wako, maana ndiye akupaye nguvu za kupata utajiri; ili alifanye imara agano lake alilowapa baba zako, kama hivi leo.
Kumbukumbu la Torati 13 : 3
3 ⑲ wewe usiyasikize maneno ya nabii yule, au yule mwotaji wa ndoto, kwa kuwa BWANA, Mungu wenu, yuawajaribu, apate kujua kwamba mwampenda BWANA, Mungu wenu, kwa mioyo yenu yote na roho zenu zote.
1 Mambo ya Nyakati 21 : 1
1 Tena shetani akasimama juu ya Israeli, akamshawishi Daudi kuwahesabu Waisraeli.
2 Mambo ya Nyakati 32 : 31
31 Lakini kuhusu wajumbe wa wakuu wa Babeli, waliotumwa kwake kuuliza ajabu iliyofanywa katika nchi, Mungu akamwacha, ili amjaribu, ili kwamba ayajue yote yaliyokuwamo moyoni mwake.
Zaburi 119 : 165
165 Wana amani nyingi waipendao sheria yako, Wala hawana la kuwakwaza.
Mithali 1 : 17
17 Kwa kuwa mtego hutegwa bure, Mbele ya macho ya ndege yeyote.
Mithali 2 : 12
12 Ili kukuokoa na njia ya uovu, Na watu wanenao yaliyopotoka;
Mithali 2 : 16
16 Ili kuokoka na malaya, Naam, malaya mwenye kubembeleza kwa maneno yake;
Mithali 4 : 15
15 Jiepushe nayo, usipite karibu nayo, Igeukie mbali, ukaende zako.
Mithali 5 : 21
21 Kwa maana njia za mwanadamu ziko mbele ya macho ya BWANA, Na mienendo yake yote huitafakari.
Mithali 6 : 28
28 Je! Mtu aweza kukanyaga makaa ya moto, Na nyayo zake zisiungue?
Mithali 7 : 23
23 Hata mshale umchome maini; Kama ndege aendaye haraka mtegoni; Wala hajui ya kuwa ni hasara ya nafsi yake.
Mithali 9 : 17
17 ⑥ Maji yaliyoibiwa ni matamu, Na mkate ulioliwa kwa siri hupendeza.
Mithali 12 : 26
26 Mwenye haki ni kiongozi wa mwenzake; Bali njia ya wasio haki huwakosesha.
Mithali 14 : 27
27 Kumcha BWANA ni chemchemi ya uzima, Ili kuepukana na tanzi za mauti.
Mithali 13 : 14
14 ⑯ Sheria ya mwenye akili ni chemchemi ya uzima, Ili kuepukana na tanzi za mauti.
Mithali 16 : 29
29 Mtu mkali humshawishi mwenzake; Humwongoza katika njia isiyo njema.
Mithali 19 : 27
27 ② Mwanangu, acha kusikia mafundisho, Ukitaka tu kuyaasi maneno ya maarifa.
Mithali 28 : 10
10 ② Kila mtu awapotezaye wenye haki katika njia mbaya, Ataanguka katika rima lake mwenyewe; Bali wakamilifu watarithi mema.
Mhubiri 7 : 26
26 Nami nimeona lililo na uchungu kupita mauti; yaani, mwanamke ambaye moyo wake ni mitego na tanzi, na mikono yake ni kama vifungo; yeye ampendezaye Mungu atamponyoka, bali mwenye dhambi atanaswa na yeye.
Isaya 33 : 16
16 Huyu ndiye atakayekaa juu; majabali ni ngome yake; atapewa chakula chake; maji yake hayatakoma.
Yeremia 2 : 25
25 Zuia mguu wako usikose kiatu, na koo yako isiwe na kiu; lakini wewe ulisema, Hakuna matumaini kabisa; la, maana nimewapenda wageni, nami nitawafuata.
Yeremia 35 : 1 – 232
1 ⑤ Neno hili ndilo lililomjia Yeremia, kutoka kwa BWANA, katika siku za Yehoyakimu, mwana wa Yosia, mfalme wa Yuda, kusema,
2 ⑥ Nenda nyumbani kwa Warekabi, ukanene nao, ukawalete nyumbani kwa BWANA, katika chumba kimoja, ukawape divai wanywe.
3 Basi nikamtwaa Yaazania, mwana wa Yeremia, mwana wa Habasinia, na ndugu zake, na wanawe wote, na nyumba yote ya Warekabi;
4 ⑦ nikawaleta ndani ya nyumba ya BWANA, ndani ya chumba cha wana wa Hanani, mwana wa Igdalia, mtu wa Mungu, kilichokuwa karibu na chumba cha wakuu, nacho kilikuwa juu ya chumba cha Maaseya, mwana wa Shalumu, bawabu;
5 nikaweka mabakuli yaliyojaa divai, na vikombe, mbele ya wana wa nyumba ya Warekabi, nikawaambia, Nyweni divai.
6 ⑧ Lakini wakasema, Hatutakunywa divai; kwa maana Yonadabu, mwana wa Rekabu, baba yetu, alituamuru, akisema, Msinywe divai, ninyi wala wana wenu, hata milele;
7 ⑩ wala msijenge nyumba, wala msipande mbegu, wala msipande mizabibu, wala msiwe nayo; bali siku zenu zote mtakaa katika hema; mpate kuishi siku nyingi katika nchi ambayo mtakaa ndani yake kama wageni.
8 ⑪ Nasi tumeitii sauti ya Yonadabu, mwana wa Rekabu, baba yetu, katika yote aliyotuamuru, kwamba tusinywe divai siku zetu zote, sisi, na wake zetu, na wana wetu, na binti zetu;
9 wala tusijijengee nyumba za kukaa; wala hatuna shamba la mizabibu, wala shamba, wala mbegu;
10 bali tumekaa katika hema, nasi tumetii; tukafanya sawasawa na yote aliyotuamuru Yonadabu, baba yetu.
11 ⑫ Lakini ikawa, Nebukadneza, mfalme wa Babeli, alipopanda akaingia nchi hii, ndipo tukasema, Haya! Twende Yerusalemu, kwa kuliogopa jeshi la Wakaldayo, na kwa kuliogopa jeshi la Washami; ndiyo maana sasa tunaishi Yerusalemu.
12 Ndipo neno la BWANA likamjia Yeremia, kusema,
13 ⑬ BWANA wa majeshi, Mungu wa Israeli, asema hivi, Nenda ukawaambie wana wa Yuda, na wenyeji wa Yerusalemu, Je! Hamtaki kupokea mafundisho, myasikilize maneno yangu? Asema BWANA.
14 ⑭ Maneno ya Yonadabu, mwana wa Rekabu, aliyowaamuru wanawe, kwamba wasinywe divai, yametimizwa, na hata leo hawanywi; maana wanaitii hiyo amri ya baba yao; lakini mimi nimesema nanyi, nikiamka mapema na kunena, bali ninyi hamkunisikiliza mimi.
15 ⑮ Pia niliwatuma watumishi wangu wote, manabii, kwenu ninyi, nikiwatuma pasipo kukoma, nikisema, Rudini sasa, kila mtu na aiache njia yake mbaya, mkatengeneze matendo yenu, wala msiifuate miungu mingine, ili kuitumikia, nanyi mtakaa katika nchi hii, niliyowapa ninyi na baba zenu; lakini hamkutega masikio yenu, wala hamkunisikiliza.
16 Basi, kwa kuwa wana wa Yonadabu, mwana wa Rekabu, wameitimiza amri ya baba yao aliyowaamuru, lakini watu hawa hawakunisikiliza mimi;
17 ⑯ kwa sababu hiyo, asema BWANA, Mungu wa majeshi, Mungu wa Israeli; Tazama nitaleta juu ya Yuda, na juu ya wenyeji wote wa Yerusalemu, mabaya yote niliyoyatamka juu yao; kwa sababu nimesema nao, wasinisikilize; nimewaita, wala hawakuniitikia.
18 ⑰ Naye Yeremia akawaambia watu wa nyumba ya Warekabi, BWANA wa majeshi, Mungu wa Israeli, asema hivi, Kwa sababu mmeitii amri ya Yonadabu, baba yenu, na kuyashika maagizo yake yote, na kutenda sawasawa na yote aliyowaamuru;
19 ⑱ basi, kwa sababu hiyo, BWANA wa majeshi, Mungu wa Israeli, asema hivi, Yonadabu, mwana wa Rekabu, hatakosa kuwa na mzawa wa kusimama mbele zangu hata milele.
Leave a Reply