Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia maisha
Warumi 6 : 23
23 Kwa maana mshahara wa dhambi ni mauti; bali karama ya Mungu ni uzima wa milele katika Kristo Yesu Bwana wetu.
Waefeso 2 : 8 – 9
8 ③ Kwa maana mmeokolewa kwa neema, kwa njia ya imani; ambayo hiyo haikutokana na nafsi zenu, ni kipawa cha Mungu;
9 ④ wala si kwa matendo, mtu awaye yote asije akajisifu.
Yohana 14 : 6
6 ⑤ Yesu akamwambia, Mimi ndimi njia, na kweli, na uzima; mtu haji kwa Baba, ila kwa njia ya mimi.
Mhubiri 7 : 1 – 29
1 Heri sifa njema kuliko manukato ya thamani; Na siku ya kufa kuliko siku ya kuzaliwa.
2 Heri kuiendea nyumba ya matanga, Kuliko kuiendea nyumba ya karamu. Kwa maana huo ndio mwisho wa wanadamu wote, naye aliye hai atautia moyoni mwake.
3 Huzuni ni afadhali kuliko kicheko, Maana simanzi ya uso ni faida ya moyo.
4 Moyo wake mwenye hekima umo nyumbani mwa matanga, bali moyo wake mpumbavu umo nyumbani mwa furaha.
5 Heri kusikia laumu ya wenye hekima, Kuliko mtu kusikia wimbo wa wapumbavu;
6 Maana kama mlio wa miiba chini ya sufuria, Ndivyo kilivyo kicheko cha mpumbavu. Hayo nayo ni ubatili.
7 Kweli jeuri humpumbaza mwenye hekima, Na rushwa huuharibu ufahamu.
8 ① Heri mwisho wa neno kuliko mwanzo wake, Na mvumilivu rohoni kuliko mwenye roho ya kiburi.
9 ② Usifanye haraka kukasirika rohoni mwako, Maana hasira hukaa kifuani mwa wapumbavu.
10 Usiseme, Kwa nini siku za kale zilikuwa ni bora kuliko siku hizi? Maana si kwa hekima unauliza hili.
11 Hekima ni njema kama urithi; Naam, nayo ni bora kwao walionalo jua.
12 Kwa maana ulinzi wa hekima ni kama ulinzi wa fedha na ubora wa maarifa ni kwamba hekima humhifadhi yeye aliye nayo.
13 ③ Tafakari vema kazi yake Mungu; kwa sababu ni nani awezaye kukinyosha kitu kile alichokipotosha yeye?
14 Siku ya kufanikiwa ufurahi, Na siku ya mabaya ufikiri. Mungu ameifanya hiyo moja kwenda sambamba na hiyo ya pili, ili mwanadamu asipate kulijua neno lolote litakalofuata baada yake.
15 ④ Mambo hayo yote nimeyaona mimi katika siku za ubatili wangu, yuko mwenye haki apoteaye katika haki yake, yuko na mtu mwovu azidishaye maisha yake katika udhalimu wake.
16 ⑤ Usiwe na haki kupita kiasi; Wala usijiongezee hekima mno; Kwa nini kujiangamiza mwenyewe?
17 ⑥ Usiwe mwovu kupita kiasi; Wala usiwe mpumbavu; Kwa nini ufe kabla ya wakati wako?
18 Ni vizuri kwamba ulishike neno hilo; naam, hata kwa neno hilo tena usiuondoe mkono wako; kwa kuwa mtu yule amchaye Mungu atatoka katika hayo yote.
19 Hekima ni nguvu zake mwenye hekima, Zaidi ya wakuu kumi waliomo mjini.
20 ⑦ Bila shaka hakuna mwanadamu mwenye haki hapa duniani, atendaye mema pasipo kutenda dhambi.
21 Tena, usitie moyoni mwako maneno yote wasemayo watu; usije ukamsikia mtumishi wako mwenyewe akikutukana.
22 Kwa kuwa mara nyingi moyo wako pia unajua ya kwamba wewe mwenyewe umewatukana watu wengine.
23 Mambo hayo yote mimi nimeyahakikisha katika hekima. Nilisema, Mimi nitakuwa na hekima, lakini imefarakana nami.
24 ⑧ Mambo yale yaliyo mbali, na yale yaendayo chini sana, ni mtu yupi awezaye kuyatafuta?
25 Nikageuka, na moyo wangu ulikazwa katika kujua na kupeleleza, na kuitafuta hekima, na maana ya mambo yaliyoko; ili nifahamu ya kuwa uovu ni upumbavu, na upumbavu ni wazimu.
26 Nami nimeona lililo na uchungu kupita mauti; yaani, mwanamke ambaye moyo wake ni mitego na tanzi, na mikono yake ni kama vifungo; yeye ampendezaye Mungu atamponyoka, bali mwenye dhambi atanaswa na yeye.
27 Tazama, asema Mhubiri, mimi nimeyaona hayo kwa kulinganisha hili na hili, ili kuitafuta jumla;
28 ambayo bado nafsi yangu ningali nikiitafuta, nisiione; mwanamume mmoja katika elfu nimemwona; bali mwanamke mmoja miongoni mwa wote mimi sikumwona.
29 ⑩ Tazama, hili tu nimeliona; Mungu amemfanya mwanadamu mnyofu, lakini wamepanga mipango mingi.
Mwanzo 2 : 7
7 BWANA Mungu akamfanya mtu kwa mavumbi ya ardhi, akampulizia puani pumzi ya uhai; mtu akawa kiumbe hai.
Waefeso 3 : 8 – 12
8 Mimi, niliye mdogo kuliko yeye aliye mdogo wa watakatifu wote, nilipewa neema hii ya kuwahubiria Mataifa utajiri wake Kristo usiopimika;
9 na kuwaangaza watu wote wajue habari za madaraka ya siri hiyo, ambayo tangu zamani zote ilisitirika katika Mungu aliyeviumba vitu vyote;
10 ili sasa, kwa njia ya kanisa, hekima ya Mungu iliyo ya namna nyingi ijulikane na falme na mamlaka katika ulimwengu wa roho;
11 kwa kadiri ya kusudi la milele alilolikusudia katika Kristo Yesu Bwana wetu.
12 Katika yeye tunao ujasiri na uwezo wa kukaribia katika tumaini kwa njia ya kumwamini.
Matendo 2 : 38
38 ⑯ Petro akawaambia, Tubuni mkabatizwe kila mmoja kwa jina lake Yesu Kristo, mpate ondoleo la dhambi zenu, nanyi mtapokea kipawa cha Roho Mtakatifu.
Leave a Reply