Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia mafuriko
Mwanzo 6 : 17
17 ④ Tazama, nitaleta gharika ya maji juu ya nchi, niharibu kila kitu chenye mwili na pumzi ya uhai, kisiwepo chini ya mbingu; kila kilichoko duniani kitakufa.
2 Petro 2 : 5
5 wala hakuuachilia ulimwengu wa kale, bali alimhifadhi Nuhu, mjumbe wa haki, na watu wengine saba, hapo alipoleta Gharika juu ya ulimwengu wa wasiomcha Mungu;
Zaburi 107 : 25 – 30
25 Maana alisema, akavumisha upepo wa dhoruba, Ukayainua juu mawimbi ya bahari.
26 ⑳ Walirushwa juu mbinguni, waliteremka hadi vilindini, Uhodari wao ukayeyuka katika maafa yao.
27 Waliyumbayumba, walipepesuka kama mlevi, Ujuzi wao wote uliwaishia.
28 Wakamlilia BWANA katika dhiki zao, Akawaponya kutoka kwa shida zao.
29 Huituliza dhoruba, ikawa shwari, Mawimbi yake yakanyamaza.
30 Ndipo walipofurahi kwa kuwa yametulia Naye akawaleta mpaka bandani waliyoitamani.
Mathayo 24 : 44
44 ⑫ Kwa sababu hiyo ninyi nanyi jiwekeni tayari; kwa kuwa katika saa msiyotazamia Mwana wa Adamu yuaja.
Luka 17 : 26
26 ② Na kama ilivyokuwa siku za Nuhu, ndivyo itakavyokuwa katika siku zake Mwana wa Adamu.
Luka 17 : 27
27 ③ Walikuwa wakila na kunywa, walikuwa wakioa na kuolewa, hata siku ile Nuhu aliyoingia katika safina, gharika ikashuka ikawaangamiza wote.
Mwanzo 8 : 20
20 Nuhu akamjengea BWANA madhabahu; akatwaa katika kila mnyama aliye safi, na katika kila ndege aliye safi, akavitoa sadaka za kuteketezwa juu ya madhabahu.
Matendo 17 : 30 – 31
30 ⑲ Basi, zamani zile za ujinga Mungu alijifanya kama hazioni; bali sasa anawaagiza watu wote wa kila mahali watubu.
31 ⑳ Kwa maana ameweka siku atakayowahukumu walimwengu kwa haki, kwa mtu yule aliyemchagua; naye amewapa watu wote uthabiti wa mambo haya kwa kumfufua katika wafu.
Leave a Reply