Biblia inasema nini kuhusu Mafumbo – Mistari yote ya Biblia kuhusu Mafumbo

Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Mafumbo

Waamuzi 9 : 15
15 Huo mti wa miiba ukaiambia miti, Ikiwa kwa kweli mnanitia mafuta niwe mfalme juu yenu, basi njoni mkakae chini ya kivuli changu; la sivyo, na utoke moto katika mti wa miiba na kuiteketeza mierezi ya Lebanoni.

2 Samweli 12 : 6
6 naye atamrudishia yule mwana-kondoo mara nne, kwa sababu ametenda neno hili, na kwa sababu hakuwa na huruma.

2 Samweli 14 : 12
12 Mwanamke akasema, Mwache mjakazi wako, nakusihi, niseme neno moja kwa bwana wangu mfalme. Akasema, Haya nena.

1 Wafalme 11 : 32
32 (lakini yeye atakuwa na kabila moja kwa ajili ya mtumishi wangu Daudi, na kwa ajili ya Yerusalemu mji ule niliouchagua katika miji yote ya makabila ya Israeli);

1 Wafalme 20 : 42
42 Akamwambia, BWANA asema hivi, Kwa sababu umemwachilia atoke mkononi mwako mtu niliyemweka ili aangamizwe kabisa, roho yako itakuwa mahali pa roho yake, na watu wako mahali pa watu wake.

2 Wafalme 14 : 9
9 ⑬ Naye Yehoashi mfalme wa Israeli akatuma kwa Amazia mfalme wa Yuda, akisema, Mbaruti uliokuwako Lebanoni ulituma kwa mwerezi uliokuwako Lebanoni, kusema, Umwoze mwanangu binti yako; kukapita hayawani aliyekuwako Lebanoni, akaukanyaga ule mbaruti.

Zaburi 80 : 16
16 Umechomwa moto; umekatwa; Kwa lawama ya uso wako wanapotea.

Isaya 5 : 7
7 Kwa maana shamba la mizabibu la BWANA wa majeshi ndilo nyumba ya Israeli, na watu wa Yuda ni mche wake wa kupendeza; akatumaini kuona hukumu ya haki, na kumbe! Aliona dhuluma; alitumaini kuona haki, na kumbe! Alisikia kilio.

Isaya 27 : 3
3 Mimi, BWANA, nililinda, Nitalitia maji kila dakika, Asije mtu akaliharibu; Usiku na mchana nitalilinda.

Isaya 28 : 29
29 ⑥ Hayo nayo yatoka kwa BWANA wa majeshi, mwenye shauri la ajabu, apitaye wote kwa hekima yake.

Yeremia 13 : 14
14 Nitawagonganisha, mtu na mwenzake, naam, baba za watu na watoto wao pamoja, asema BWANA; sitahurumia, wala sitaachilia, wala sitarehemu, hata nisiwaangamize.

Ezekieli 15 : 8
8 Nami nitaifanya nchi kuwa ukiwa, kwa sababu wamekosa, asema Bwana MUNGU.

Ezekieli 17 : 10
10 Naam, tazama, ingawa umepandwa, je! Utafanikiwa? Hautakauka kabisa, upepo wa mashariki utakapoupiga? Naam, utakauka katika matuta hapo ulipopandwa.

Ezekieli 19 : 14
14 Na moto umetoka katika vijiti vya matawi yake, umekula matunda yake, hata hana tena kijiti cha nguvu kifaacho kwa fimbo ya enzi ya kutawala. Na hayo ni maombolezo, nayo yatakuwa maombolezo.

Ezekieli 19 : 9
9 Wakamtia katika tundu kwa kulabu, wakamleta kwa mfalme wa Babeli wakamtia ndani ya ngome, sauti yake isisikiwe tena juu ya milima ya Israeli.

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *