Biblia inasema nini kuhusu Madhabahu – Mistari yote ya Biblia kuhusu Madhabahu

Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Madhabahu

Mwanzo 8 : 20
20 Nuhu akamjengea BWANA madhabahu; akatwaa katika kila mnyama aliye safi, na katika kila ndege aliye safi, akavitoa sadaka za kuteketezwa juu ya madhabahu.

Mwanzo 12 : 8
8 Kisha akaondoka huko akaenda mpaka mlima ulio upande wa mashariki wa Betheli, akaipiga hema yake; Betheli ilikuwa upande wa magharibi, na Ai upande wa mashariki, akamjengea BWANA madhabahu huko, akaliitia jina la BWANA.

Mwanzo 13 : 18
18 Basi Abramu akahamisha hema yake, akaja na kukaa karibu na mialoni ya Mamre, nayo ni miti iliyoko Hebroni, akamjengea BWANA madhabahu huko.

Mwanzo 22 : 9
9 Wakafika mahali pale alipoambiwa na Mungu, Abrahamu akajenga madhabahu huko, akaziweka tayari kuni, kisha akamfunga Isaka mwanawe, akamweka juu ya madhabahu, juu ya zile kuni.

Mwanzo 26 : 25
25 ④ Akajenga madhabahu huko, akaliitia jina la BWANA. Akapiga hema yake huko, na watumwa wa Isaka wakachimba kisima huko.

Mwanzo 33 : 20
20 Akajenga huko madhabahu, akaiita, El-elohe-Israeli.[16]

Mwanzo 35 : 7
7 ⑩ Akajenga huko madhabahu, akapaita mahali pale, El-Betheli; kwa sababu huko Mungu alimtokea, hapo alipomkimbia ndugu yake.

Kutoka 17 : 15
15 Musa akajenga madhabahu, akaiita jina lake Yahweh-nisi;[21]

Kutoka 24 : 4
4 ⑮ Basi Musa akayaandika maneno yote ya BWANA, akaondoka asubuhi na mapema, akajenga madhabahu chini ya mlima, na nguzo kumi na mbili, kwa hesabu ya makabila kumi na mawili ya Israeli,

Hesabu 23 : 1
1 Balaamu akamwambia Balaki, Nijengee hapa madhabahu saba, ukaniandalie hapa ng’ombe dume saba, na kondoo dume saba.

Hesabu 23 : 14
14 ③ Akamchukua mpaka shamba la Sofimu, hadi kilele cha Pisga, akajenga madhabahu saba, akatoa sadaka ng’ombe dume mmoja na kondoo dume mmoja juu ya kila madhabahu.

Hesabu 23 : 29
29 ⑫ Balaamu akamwambia Balaki, Haya, unijengee hapa madhabahu saba, kisha uniandalie ng’ombe dume saba, na kondoo dume saba.

Kumbukumbu la Torati 27 : 7
7 ufanye na sadaka za amani, ukale huko; nawe furahi mbele za BWANA, Mungu wako.

Yoshua 8 : 32
32 ① Akaandika huko juu ya mawe hayo nakala ya Torati ya Musa, aliyoiandika mbele ya wana wa Israeli.

Yoshua 22 : 10
10 Nao walipofika pande za Yordani[9] zilizo katika nchi ya Kanaani, hao wana wa Reubeni, na wana wa Gadi, na nusu ya kabila la Manase, wakajenga madhabahu huko karibu na Yordani, iliyoonekana kuwa ni madhabahu kubwa.

Yoshua 22 : 34
34 Basi hao wana wa Reubeni, na wana wa Gadi, wakaiita madhabahu hiyo Edi; wakasema, Kwa kuwa ni ushahidi kati yetu ya kwamba yeye BWANA ndiye Mungu.

Waamuzi 6 : 27
27 Ndipo Gideoni akatwaa watu kumi miongoni mwa watumishi wake, akafanya kama BWANA alivyomwambia; lakini kwa kuwa aliwaogopa watu wa nyumba ya baba yake, na watu wa mji, hakuweza kuyatenda hayo wakati wa mchana, basi aliyatenda usiku.

1 Samweli 7 : 17
17 Kisha alikuwa akirudi Rama; maana ndipo ilipokuwa nyumba yake; nako ndiko alikowaamua Waisraeli; na huko akamjengea BWANA madhabahu.

1 Samweli 14 : 35
35 Naye Sauli akamjengea BWANA madhabahu; hiyo ndiyo madhabahu ya kwanza aliyomjengea BWANA.

2 Samweli 24 : 19
19 Basi Daudi akakwea kama alivyoagizwa na Gadi, kama BWANA alivyoamuru.

1 Wafalme 18 : 32
32 Naye akaijenga madhabahu kwa mawe hayo katika jina la BWANA; akafanya mfereji, kama wa vipimo viwili vya mbegu, ukiizunguka madhabahu.

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *