Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Mabara
Mwanzo 1 : 10
10 Mungu akapaita pale pakavu Nchi; na makusanyiko ya maji akayaita Bahari; Mungu akaona ya kuwa ni vyema.
Ayubu 26 : 7
7 ⑯ Yeye hutandaza kaskazi juu ya nafasi isiyo na kitu, Na kuutundika ulimwengu pasipo kitu.
Ayubu 26 : 10
10 ⑱ Amepiga duara kuwa ni mpaka juu ya uso wa maji, Hata hapo mwanga na giza vinapopakana.
Ayubu 28 : 11
11 Hufunga vijito visichuruzike; Na kitu kilichositirika hukifunua.
Ayubu 38 : 18
18 Umeyafahamu mapana ya dunia? Haya! Sema, ikiwa unayajua hayo yote.
Zaburi 95 : 5
5 Bahari ni yake, ndiye aliyeifanya, Na mikono yake iliumba nchi kavu.
Zaburi 104 : 9
9 ⑳ Umeweka mpaka yasiupite, Wala yasirudi kuifunikiza nchi.
Zaburi 136 : 6
6 Yeye aliyeitandaza nchi juu ya maji; Kwa maana fadhili zake ni za milele.
Mithali 8 : 29
29 Alipoipa bahari mpaka wake, Kwamba maji yake yasiasi amri yake; Alipoiagiza misingi ya nchi;
Leave a Reply