Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Lugha
Mwanzo 11 : 1
1 ⑱ Nchi yote ilikuwa na lugha moja na usemi mmoja.
Mwanzo 11 : 6
6 BWANA akasema, Tazama, watu hawa ni taifa moja, na lugha yao ni moja; na haya ndiyo wanayoanza kuyafanya, wala sasa hawatazuiliwa neno wanalokusudia kulifanya.
Mwanzo 11 : 9
9 Kwa sababu hiyo jina lake likaitwa Babeli; maana hapo ndipo BWANA alipoichafua lugha ya dunia yote; na kutoka huko BWANA akawatawanya waende usoni pa nchi yote.
Mwanzo 10 : 5
5 Kwa hao nchi za pwani za mataifa ziligawanyikana kuwa nchi zao, kila moja kwa lugha yake, kwa jamaa zao, kufuata mataifa yao.
Mwanzo 10 : 20
20 Hao ndio wana wa Hamu, kufuata jamaa zao, kwa lugha zao, katika nchi zao, kufuata mataifa yao.
Mwanzo 10 : 31
31 Hao ndio wana wa Shemu, kufuata jamaa zao, na lugha zao, katika nchi zao, kufuata mataifa yao.
Waamuzi 12 : 6
6 ndipo walipomwambia, Haya, tamka sasa neno hili, Shibolethi; naye akasema, Sibolethi; kwa maana hakuweza kufanya midomo yake kutamka neno hilo sawasawa; ndipo wakamshika, na kumwua hapo penye vivuko vya Yordani; basi wakaanguka watu elfu arubaini na mbili wa Efraimu wakati huo.
Mathayo 26 : 73
73 Punde kidogo, wale waliokuwapo wakamwendea, wakamwambia Petro, Hakika wewe nawe u mmoja wao; kwa sababu hata usemi wako wakutambulisha.
Yohana 19 : 20
20 Basi anwani hiyo waliisoma wengi katika Wayahudi; maana mahali pale aliposulubiwa Yesu palikuwa karibu na mji; nayo iliandikwa kwa Kiebrania, na Kirumi, na Kigiriki.
Matendo 2 : 11
11 Wakrete na Waarabu; tunawasikia hawa wakisema kwa lugha zetu matendo makuu ya Mungu.
1 Wakorintho 14 : 28
28 Lakini asipokuwapo mwenye kufasiri na anyamaze katika kanisa; aseme na nafsi yake tena na Mungu.
Marko 16 : 17
17 ③ Na ishara hizi zitafuatana na hao waaminio; kwa jina langu watatoa pepo; watasema kwa lugha mpya;
Matendo 2 : 8
8 Imekuwaje basi sisi kusikia kila mtu lugha yetu tuliyozaliwa nayo?
Matendo 10 : 46
46 ⑰ Kwa maana waliwasikia wakisema kwa lugha, na kumwadhimisha Mungu. Ndipo Petro akajibu,
Matendo 19 : 6
6 Na Paulo, alipokwisha kuweka mikono yake juu yao, Roho Mtakatifu akaja juu yao; wakaanza kunena kwa lugha, na kutabiri.
1 Wakorintho 12 : 10
10 na mwingine matendo ya miujiza; na mwingine unabii; na mwingine kupambanua roho; mwingine aina za lugha; na mwingine fasiri za lugha;
Nehemia 13 : 24
24 na nusu ya watoto wao wakazungumza kwa lugha ya Ashdodi, wala hawakuweza kuzungumza Kiyahudi, bali kwa lugha mojawapo ya watu hao.
Danieli 1 : 4
4 vijana wasio na kasoro, wazuri wa uso, wajuzi wa hekima, werevu kwa sababu ya maarifa yao, wenye kufahamu elimu, watakaoweza kusimama katika jumba la mfalme; tena alimwambia awafundishe kusoma na kuandika, lugha ya Wakaldayo.
Matendo 2 : 10
10 Frigia na Pamfilia, Misri na pande za Libya karibu na Kirene, na wageni watokao Rumi, Wayahudi na waongofu,
Zaburi 114 : 1 – 104
1 Haleluya. Israeli alipotoka Misri, Na Yakobo katika watu wa lugha ya kigeni.
2 Yuda ilikuwa patakatifu pake, Israeli milki yake.
3 Bahari iliona ikakimbia, Yordani ilirudishwa nyuma.
4 Milima iliruka kama kondoo dume, Vilima kama wana-kondoo.
5 Ee bahari, una nini, ndio ukimbie? Yordani, ndio urudi nyuma?
6 Enyi milima, ndio mruke kama kondoo dume? Enyi vilima, kama wana-kondoo?
7 Tetemeka, Ee nchi, mbele za uso wa Bwana, Mbele za uso wa Mungu wa Yakobo.
8 Augeuzaye mwamba kuwa ziwa la maji, Jiwe gumu kuwa chemchemi.
Leave a Reply