Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Lin
Kutoka 9 : 31
31 ⑤ Kitani na shayiri zilipigwa; maana shayiri zilikuwa na masuke na kitani zilikuwa katika kutoa maua.
Yoshua 2 : 6
6 Lakini yeye alikuwa amewapandisha darini, akawaficha kwa mabua ya kitani, aliyokuwa ameyatandika juu ya dari.
Mithali 31 : 13
13 Hutafuta sufu na kitani; Hufanya kazi yake kwa moyo wote.
Isaya 19 : 6
6 ① Na vijito vya mto vitatoa uvundo, na mifereji ya Misri itakuwa haina maji mengi, itakauka; manyasi na mianzi itanyauka.
Hosea 2 : 5
5 Maana mama yao amezini; yeye aliyewachukua mimba ametenda mambo ya aibu; maana alisema, Nitafuatana na wapenzi wangu, wanipao chakula changu na maji yangu, sufu yangu na kitani yangu, mafuta yangu na vileo vyangu.
Hosea 2 : 9
9 Basi kwa ajili ya hayo, nitaitwaa tena ngano yangu kwa wakati wake, na divai yangu kwa wakati wake, nami nitamnyang’anya sufu yangu na kitani yangu, vya kumfunika uchi wake.
Esta 1 : 16
16 Basi Memukani akajibu mbele ya mfalme na wakuu, Huyu Vashti, malkia, hakumkosa mfalme tu peke yake, ila na wakuu wote, na watu wote pia walioko katika majimbo yote ya mfalme Ahasuero.
Isaya 42 : 3
3 Mwanzi uliopondeka hatauvunja, wala utambi utokao moshi hatauzima; atatoa hukumu kwa uaminifu.
Mathayo 12 : 20
20 Mwanzi uliopondeka hatauvunja, Wala utambi utokao moshi hatauzima, Hadi ailetapo hukumu ikashinda.
Leave a Reply