Biblia inasema nini kuhusu Kuzingirwa – Mistari yote ya Biblia kuhusu Kuzingirwa

Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Kuzingirwa

Kumbukumbu la Torati 20 : 12
12 Na kwamba hautaki kufanya amani nawe, lakini utafanya vita juu yako, ndipo uuhusuru;

Kumbukumbu la Torati 20 : 20
20 Ila miti uijuayo si miti ya kuliwa iangamize, na kuitema; ukajenge maburuji juu ya mji ufanyao vita juu yako, hata uanguke.

Isaya 29 : 3
3 Nami nitapiga kimo juu yako pande zote, nitakuhusuru kwa ngome, nami nitajenga maboma yakuzunguke.

2 Wafalme 6 : 29
29 Basi, tukamtokosa mtoto wangu, tukamla; nikamwambia siku ya pili, Mtoe mtoto wako, tumle; naye amemficha mtoto wake.

2 Wafalme 25 : 3
3 Siku ya tisa ya mwezi wa nne njaa ilikuwa nzito ndani ya mji, hata hapakuwa na chakula kwa watu wa nchi.

Isaya 9 : 20
20 ⑪ Hupokonya upande wa mkono wa kulia, nao huona njaa! Hula upande wa mkono wa kushoto, wala hawashibi! Watakula kila mtu nyama ya mkono wake mwenyewe.

Isaya 36 : 12
12 Lakini yule kamanda akawaambia, Je! Bwana wangu amenituma niseme, maneno haya kwa bwana wako na kwako wewe? Hakunituma pia kwa watu hawa wanaokaa ukutani, wanaokabiliwa na tisho la kula mavi yao wenyewe na kunywa mkojo wao pamoja nanyi?

Yeremia 19 : 9
9 Nami nitawalazimisha kula nyama ya wana wao, na nyama ya binti zao, nao watakula kila mmoja nyama ya rafiki yake, wakati wa mazingira na dhiki, ambayo adui zao, na watu wale watafutao roho zao, watawatesa.

2 Wafalme 6 : 29
29 Basi, tukamtokosa mtoto wangu, tukamla; nikamwambia siku ya pili, Mtoe mtoto wako, tumle; naye amemficha mtoto wake.

2 Samweli 11 : 1
1 Hata ikawa, mwanzo wa mwaka mpya, wakati watokapo wafalme kwenda vitani, Daudi akamtuma Yoabu, na watumishi wake pamoja naye, na Israeli wote; wakawaangamiza Waamoni, wakauzingira Raba. Lakini Daudi mwenyewe akakaa Yerusalemu.

2 Samweli 20 : 15
15 ⑲ Na hao wakaja wakauzingira katika Abeli wa Bethmaaka, wakafanya kilima mbele ya mji, nacho kikasimama kuielekea ngome; na watu wote waliokuwa pamoja na Yoabu wakavunjavunja ukuta, wapate kuubomoa.

1 Wafalme 15 : 27
27 Basi Baasha wa Ahiya, wa ukoo wa Isakari, akamfanyia fitina; Baasha akampiga huko Gibethoni ulio wa Wafilisti; kwani Nadabu na Israeli wote walikuwa wakiuhusuru Gibethoni.

1 Wafalme 16 : 17
17 Omri akapanda kutoka Gibethoni, na Israeli wote pamoja naye, wakauhusuru Tirza.

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *