Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Kuzimu
Mathayo 10 : 28
28 ⑤ Msiwaogope wauuao mwili, wasiweze kuiua na roho; afadhali mwogopeni yule awezaye kuangamiza mwili na roho pia katika Jehanamu.
Mathayo 11 : 23
23 Nawe Kapernaumu, je! Utakuzwa mpaka mbinguni? Utashushwa mpaka kuzimu; kwa kuwa kama miujiza iliyofanyika kwako ingalifanyika katika Sodoma, ungalikuwapo mji huo hata leo.
Mathayo 16 : 18
18 ⑯ Nami nakuambia, Wewe ndiwe Petro, na juu ya mwamba huu nitalijenga kanisa langu; wala milango ya kuzimu haitalishinda.
Luka 10 : 15
15 Nawe Kapernaumu, je! Utakuzwa hata mbinguni? Utashushwa hata kuzimu.
Luka 16 : 23
23 Basi, kule kuzimu aliyainua macho yake, alipokuwa katika mateso, akamwona Abrahamu kwa mbali, na Lazaro kifuani mwake.
Matendo 2 : 27
27 ⑦ Kwa maana hutaiacha roho yangu katika kuzimu; Wala hutamtoa Mtakatifu wako aone uharibifu.
Matendo 2 : 31
31 ⑪ yeye mwenyewe akitangulia kuyaona haya, alitaja habari za kufufuka kwake Kristo, ya kwamba roho yake haikuachwa kuzimu, wala mwili wake haukuona uharibifu.
Ufunuo 1 : 18
18 na aliye hai; nami nilikuwa nimekufa, na tazama, ni hai hata milele na milele. Nami ninazo funguo za mauti, na za kuzimu.
Ufunuo 6 : 8
8 ⑧ Nikaona, na tazama, farasi wa rangi ya kijivujivu, na yeye aliyempanda jina lake ni Mauti, na Kuzimu akafuatana naye. Nao wakapewa mamlaka juu ya robo ya nchi, waue kwa upanga na kwa njaa na kwa tauni na kwa wanyama wa nchi.
2 Samweli 22 : 6
6 Kamba za kuzimu zilinizunguka; Mitego ya mauti ikanikabili.
Ayubu 26 : 5
5 Hao waliokufa watetemesha Chini ya maji na hao wakaamo humo.
Zaburi 6 : 5
5 ⑤ Maana mautini hapana kumbukumbu lako; Katika kuzimu ni nani atakayekushukuru?
Zaburi 17 : 15
15 ⑥ Bali mimi nikutazame uso wako katika haki, Niamkapo nishibishwe kwa sura yako.
Zaburi 30 : 9
9 ⑯ Mna faida gani katika damu yangu Nishukapo Shimoni? Mavumbi yatakusifu? Yatautangaza uaminifu wako?
Zaburi 49 : 15
15 Bali Mungu atanikomboa nafsi yangu, Atanitoa mkononi mwa kuzimu, maana atanipokea.
Zaburi 86 : 13
13 Maana fadhili zako kwangu ni nyingi sana; Umeiopoa nafsi yangu na kuzimu.
Zaburi 88 : 12
12 Miujiza yako itajulikana gizani? Au haki yako katika nchi ya usahaulifu?
Zaburi 115 : 17
17 Wafu hawamsifu Mungu BWANA, Wala yeyote ashukaye kwenye kimya;
Zaburi 116 : 3
3 Kamba za mauti zilinizunguka, Shida za kuzimu zilinipata. Nilipata dhiki na mateso;
Mithali 15 : 24
24 ③ Kwa mtu mwenye akili njia ya uhai huenda juu; Ili atoke katika kuzimu chini.
Mithali 21 : 16
16 Mtu aikosaye njia ya busara Atakaa katika mkutano wao waliokufa.
Mithali 27 : 20
20 Kuzimu na Uharibifu havishibi; Wala macho ya wanadamu hayashibi.
Leave a Reply