Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia kuwatumikia mabwana wawili
Luka 16 : 13
13 Hakuna mtumishi awezaye kutumikia mabwana wawili; kwa maana, ama atamchukia huyu na kumpenda huyu, ama atashikamana na huyu na kumdharau huyu. Hamwezi kumtumikia Mungu na mali.
Mathayo 6 : 24
24 ③ Hakuna mtu awezaye kutumikia mabwana wawili; kwa maana atamchukia huyu, na kumpenda huyu; ama atashikamana na huyu, na kumdharau huyu. Hamwezi kumtumikia Mungu na mali.
Zaburi 45 : 7
7 ⑧ Umeipenda haki; Umeichukia dhuluma. Kwa hiyo MUNGU, Mungu wako, amekutia mafuta, Mafuta ya furaha kuliko wenzako.
Kumbukumbu la Torati 4 : 24
24 kwa kuwa BWANA, Mungu wenu, ni moto uangamizao, Mungu mwenye wivu.
Leave a Reply