Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia kutoa pesa
2 Wakorintho 9 : 7
7 Kila mtu na atende kama alivyokusudia moyoni mwake, si kwa huzuni, wala si kwa lazima; maana Mungu humpenda yeye atoaye kwa moyo mkunjufu.
Mithali 19 : 17
17 Amhurumiaye maskini humkopesha BWANA; Naye atamlipa kwa tendo lake jema.
Marko 12 : 41 – 44
41 ⑱ Naye akaketi kulielekea sanduku la hazina, akatazama jinsi mkutano watiavyo mapesa katika sanduku. Matajiri wengi wakatia mengi.⑲
42 Akaja mwanamke mmoja, mjane, maskini, akatia senti mbili, kiasi cha nusu pesa.
43 Akawaita wanafunzi wake, akawaambia, Amin, nawaambia, Huyu mjane maskini ametia zaidi kuliko wote wanaotia katika sanduku la hazina;
44 ⑳ maana hao wote walitia baadhi ya mali iliyowazidi; bali huyu katika umaskini wake ametia vyote alivyokuwa navyo, ndiyo riziki yake yote pia.
Luka 6 : 38
38 Wapeni watu vitu, nanyi mtapewa; kipimo cha kujaa na kushindiliwa, na kusukwasukwa hata kumwagika, ndicho watu watakachowapa vifuani mwenu. Kwa kuwa kipimo kile kile mpimacho ndicho mtakachopimiwa.
Mathayo 6 : 1 – 4
1 Angalieni msifanye wema wenu machoni pa watu, kusudi mtazamwe na wao; kwa maana mkifanya kama hayo, hampati thawabu kwa Baba yenu aliye mbinguni.
2 Basi wewe utoapo sadaka, usipige panda mbele yako, kama wanafiki wafanyavyo katika masinagogi na njiani, ili watukuzwe na watu.
3 Amin, nawaambieni, Wamekwisha kupata thawabu yao. Bali wewe utoapo sadaka, hata mkono wako wa kushoto usijue ufanyalo mkono wako wa kulia;
4 sadaka yako iwe kwa siri; na Baba yako aonaye sirini atakujazi.
Matendo 20 : 35
35 Katika mambo yote nimewaonesha ya kuwa kwa kushika kazi hivi imewapasa kuwasaidia wanyonge, na kuyakumbuka maneno ya Bwana Yesu, jinsi alivyosema mwenyewe, Ni heri kutoa kuliko kupokea.
Mathayo 6 : 33
33 ⑩ Bali utafuteni kwanza ufalme wake, na haki yake; na hayo yote mtazidishiwa.
Kumbukumbu la Torati 15 : 7 – 11
7 ② Kama akiwapo mtu maskini pamoja nawe, nduguzo mmojawapo, ndani ya malango yako mojawapo, katika nchi yako akupayo BWANA, Mungu wako, usifanye moyo wako kuwa mgumu, wala usimfumbie mkono wako nduguyo maskini;
8 ③ lakini mfumbulie mkono wako kwa kweli, umkopeshe kwa kweli yatoshayo haja yake katika ahitajiayo.
9 ④ Jitunze, msiwe na neno lisilofaa moyoni mwako, kusema, Umekaribia mwaka wa saba, mwaka wa maachilio; jicho lako likawa ovu juu ya nduguyo usimpe kitu; naye akamlilia BWANA juu yako, ikawa ni dhambi kwako.
10 ⑤ Mpe kwa kweli, wala moyo wako usisikitike utakapompa; kwa kuwa atakubarikia BWANA, Mungu wako, kwa neno hili katika kazi yako yote, na katika kila utakalotia mkono wako.
11 ⑥ Kwa maana maskini hawatakoma katika nchi milele; ndipo ninakuamuru na kukuambia, Mfumbulie kwa kweli mkono wako nduguyo, mhitaji wako, maskini wako, katika nchi yako.
1 Timotheo 5 : 8
8 Lakini mtu yeyote asiyewatunza walio wake, yaani, wale wa nyumbani mwake hasa, ameikana imani, tena ni mbaya kuliko mtu asiyeamini.
Mithali 20 : 21
21 ⑫ Urithi uliopatikana mwanzo kwa haraka, Mwisho wake, lakini, hautabarikiwa.
Waraka kwa Waebrania 13 : 5
5 Msiwe na tabia ya kupenda fedha; muwe radhi na vitu mlivyo navyo; kwa kuwa yeye mwenyewe amesema, Sitakupungukia kamwe, wala sitakuacha.
Kumbukumbu la Torati 8 : 18
18 ⑳ Bali utamkumbuka BWANA, Mungu wako, maana ndiye akupaye nguvu za kupata utajiri; ili alifanye imara agano lake alilowapa baba zako, kama hivi leo.
Mithali 3 : 9 – 10
9 ⑥ Mheshimu BWANA kwa mali yako, Na kwa malimbuko ya mazao yako yote.
10 ⑦ Ndipo ghala zako zitakapojazwa kwa wingi, Na vyombo vyako vitafurika divai mpya.
Mithali 22 : 7
7 Tajiri humtawala maskini, Naye akopaye ni mtumwa wake akopeshaye.
2 Wakorintho 8 : 13
13 Maana sisemi hayo, ili wengine wapate raha nanyi mpate dhiki;
Waraka kwa Waebrania 13 : 15 – 16
15 ⑤ Basi, kwa njia yake yeye, na tumpe Mungu dhabihu ya sifa daima, yaani, tunda la midomo iliungamalo jina lake.
16 ⑥ Lakini msisahau kutenda mema na kushirikiana; maana sadaka kama hizi ndizo zimpendezazo Mungu.
2 Wakorintho 8 : 7
7 Lakini kama mlivyo na wingi wa mambo yote; imani, na usemi, na elimu, na bidii yote, na upendo wenu kwetu sisi; basi vivyo hivyo mpate wingi wa neema hii pia.
1 Timotheo 6 : 10
10 Maana shina moja la mabaya ya kila namna ni kupenda fedha; ambayo wengine hali wakiitamani hiyo wamefarakana na Imani, na kujichoma kwa maumivu mengi.
Malaki 3 : 8 – 12
8 ② Je! Mwanadamu atamwibia Mungu? Lakini ninyi mnaniibia mimi. Lakini ninyi mwasema, Tumekuibia kwa namna gani? Mmeniibia zaka na dhabihu.
9 Ninyi mmelaaniwa kwa laana; maana mnaniibia mimi, naam, taifa hili lote.
10 ③ Leteni zaka kamili ghalani, ili kiwemo chakula katika nyumba yangu, mkanijaribu kwa njia hiyo, asema BWANA wa majeshi; mjue kama sitawafungulia madirisha ya mbinguni, na kuwamwagieni baraka, hata isiwepo nafasi ya kutosha, au la.
11 ④ Nami kwa ajili yenu nitamkemea yeye alaye, wala hataharibu mazao ya ardhi yenu; wala mzabibu wenu hautapukutisha matunda yake kabla ya wakati wake katika mashamba, asema BWANA wa majeshi.
12 ⑤ Na mataifa yote watawaiteni heri; maana mtakuwa nchi ya kupendeza sana, asema BWANA wa majeshi.
Luka 21 : 1 – 360
1 Akainua macho yake akawaona matajiri wakitia sadaka zao katika sanduku la hazina.
2 Akamwona mjane mmoja maskini akitia mle senti mbili.
3 Akasema, Hakika nawaambia, huyu mjane maskini ametia zaidi kuliko wote;
4 maana, hao wote walitoa sadaka katika mali iliyowazidi, bali huyu katika umaskini wake ametia vyote alivyokuwa navyo.
5 Na watu kadhaa walipokuwa wakiongea habari za hekalu, jinsi lilivyopambwa kwa mawe mazuri na sadaka za watu, alisema,
6 Haya mnayoyatazama, siku zitakuja ambapo halitasalia jiwe juu ya jiwe ambalo halitabomolewa.
7 Wakamwuliza wakisema, Mwalimu, mambo hayo yatakuwa lini? Nayo ni nini ishara ya kuwa mambo hayo yako karibu kutukia?
8 Akasema, Angalieni, msije mkadanganyika, kwa sababu wengi watakuja kwa jina langu, wakisema, Mimi ndiye; tena, Majira yamekaribia. Basi msiwafuate hao.
9 Nanyi mtakaposikia habari za vita na fitina, msitishwe; maana, hayo hayana budi kutukia kwanza, lakini ule mwisho hauji upesi.
10 Kisha aliwaambia, Taifa litaondoka kupigana na taifa, na ufalme kupigana na ufalme;
11 kutakuwa na mitetemeko mikubwa ya ardhi; na njaa na tauni mahali pengi; na mambo ya kutisha na ishara kuu kutoka mbinguni.
12 Lakini, kabla hayo yote hayajatokea, watawakamata na kuwaudhi; watawapeleka mbele ya masinagogi, na kuwaua magerezani, mkipelekwa mbele ya wafalme na watawala kwa ajili ya jina langu.
13 Na hayo yatakuwa ushuhuda kwenu.
14 Basi, kusudieni mioyoni mwenu, kutofikiri-fikiri kwanza mtakavyojibu;
15 kwa sababu mimi nitawapa kinywa na hekima ambayo watesi wenu wote hawataweza kushindana nayo wala kuipinga.
16 Nanyi mtasalitiwa na wazazi wenu, na ndugu zenu, na jamaa zenu, na rafiki zenu, nao watawaua baadhi yenu.
17 Nanyi mtachukiwa na watu wote kwa ajili ya jina langu.
18 Lakini hautapotea hata unywele mmoja wa vichwa vyenu.
19 Nanyi kwa subira yenu mtaziponya nafsi zenu.
20 Lakini, hapo mtakapoona mji wa Yerusalemu umezungukwa na majeshi, basi jueni ya kwamba uharibifu wake umekaribia.
21 Ndipo walio katika Yudea na wakimbilie milimani, na walio katikati yake wakimbilie nje, na walio katika mashamba wasiuingie.
22 Kwa kuwa siku hizo ndizo za mapatilizo, ili yatimizwe yote yaliyoandikwa.
23 Ole wao wenye mimba na wanaonyonyesha katika siku hizo! Kwa kuwa kutakuwa na shida nyingi katika nchi, na hasira juu ya taifa hili.
24 Wataanguka kwa ukali wa upanga, nao watatekwa nyara na kuchukuliwa katika mataifa yote; na Yerusalemu utakanyagwa na Mataifa, hadi majira ya Mataifa yatakapotimia.
25 Tena, kutakuwa na ishara katika jua, na mwezi, na nyota; na katika nchi dhiki ya mataifa wakishangaa kwa kuvuma kwa habari na mawimbi yake;
26 watu wakivunjika mioyo kwa hofu, na kwa kutazamia mambo yatakayoupata ulimwengu. Kwa kuwa nguvu za mbinguni zitatikisika.
27 Hapo ndipo watakapomwona Mwana wa Adamu akija katika wingu pamoja na nguvu na utukufu mwingi.
28 Basi mambo hayo yaanzapo kutokea, changamkeni, mkaviinue vichwa vyenu, kwa kuwa ukombozi wenu umekaribia.
29 Akawaambia mfano; Utazameni mtini na miti mingine yote.
30 Wakati imalizapo kuchipuka, mwaona na kutambua wenyewe ya kwamba majira ya mavuno yamekwisha kuwa karibu.
31 Nanyi kadhalika, mwonapo mambo hayo yanaanza kutokea, tambueni ya kwamba ufalme wa Mungu u karibu.
32 Amin, nawaambieni, Kizazi hiki hakitapita kabla ya hayo yote kutimia.
33 Mbingu na nchi zitapita, lakini maneno yangu hayatapita kamwe.
34 Basi, jihadharini, mioyo yenu isije ikalemewa na ulafi, na ulevi, na masumbufu ya maisha haya; siku ile ikawajia ghafla, kama mtego unasavyo;
35 kwa kuwa ndivyo itakavyowajia watu wote wakaao juu ya uso wa dunia nzima.
36 ① Basi, kesheni ninyi kila wakati, mkiomba, ili mpate kuokoka katika haya yote yatakayotokea, na kusimama mbele za Mwana wa Adamu.
37 ② Basi, kila mchana alikuwa akifundisha hekaluni, na usiku huenda kulala katika mlima uitwao wa Mizeituni.
38 Na watu wote walikuwa wakiamka mapema waende hekaluni ili kumsikiliza.
Leave a Reply