Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia kusubiri
Maombolezo 3 : 25
25 BWANA ni mwema kwa hao wamngojeao, Kwa hiyo nafsi imtafutayo.
Zaburi 27 : 14
14 ② Umtumainie BWANA, uwe imara, Upige moyo konde, naam, umngoje BWANA.
Zaburi 39 : 7
7 Na sasa ninangoja nini, Ee Bwana? Matumaini yangu ni kwako.
Habakuki 2 : 3
3 Maana njozi hii bado ni kwa wakati ulioamriwa, inafanya haraka ili kuufikia mwisho wake, wala haitasema uongo; ijapokawia, ingojee; kwa kuwa haina budi kuja, haitakawia.
Zaburi 37 : 7
7 Utulie mbele za BWANA, Nawe umngojee kwa subira; Usihangaike juu ya afanikiwaye katika njia yake, Wala mtu apangaye maovu.
Mika 7 : 7
7 Lakini mimi, nitamtazamia BWANA; nitamngojea Mungu wa wokovu wangu; Mungu wangu atanisikia.
Isaya 40 : 31
31 bali wao wamngojeao BWANA watapata nguvu mpya; watapanda juu kwa mbawa kama tai; watakimbia, wala hawatachoka; watakwenda kwa miguu, wala hawatazimia.
Zaburi 62 : 5
5 Nafsi yangu, umngoje Mungu peke yake kwa utulivu. Maana tumaini langu hutoka kwake.
Isaya 30 : 18
18 Kwa ajili ya hayo BWANA atangoja, ili awaonee huruma, na kwa ajili ya hayo atatukuzwa, ili awarehemu; kwa maana BWANA ni Mungu wa hukumu; heri wote wamngojao.
Zaburi 33 : 20
20 Nafsi zetu zinamngoja BWANA; Yeye ndiye msaada wetu na ngao yetu.
Zaburi 59 : 9
9 Ee nguvu zangu, nitakungoja Wewe, Maana Mungu ndiye aliye ngome yangu.
Isaya 33 : 2
2 Ee BWANA, uturehemu; tumekungoja wewe; uwe wewe mkono wetu[7] kila asububi, na wokovu wetu pia wakati wa taabu.
Zaburi 52 : 9
9 ⑯ Nitakushukuru milele kwa maana umetenda; Nitalingojea jina lako kwa kuwa ni jema; Mbele ya wacha Mungu wako.
Zaburi 25 : 21
21 Ukamilifu na unyofu zinihifadhi, Maana nakungoja Wewe.
Zaburi 62 : 2
2 Yeye tu ndiye mwamba wangu na wokovu wangu, Ngome yangu, sitatikisika.
Yakobo 5 : 7
7 Kwa hiyo ndugu, vumilieni, hata kuja kwake Bwana. Tazama, mkulima hungoja mazao ya nchi yaliyo ya thamani, huvumilia kwa ajili yake hata yatakapopata mvua ya kwanza na ya mwisho.
Isaya 64 : 4
4 ⑯ Maana tangu zamani za kale watu hawakusikia, wala kufahamu kwa masikio, wala jicho halikuona Mungu, ila wewe, atendaye mambo kwa ajili yake amngojaye.
Isaya 49 : 23
23 Na wafalme watakuwa baba zako walezi, na malkia zao mama zako walezi; watainama mbele yako kifudifudi, na kuramba mavumbi ya miguu yako; nawe utajua ya kuwa mimi ni BWANA, tena waningojeao hawatatahayarika.
Zaburi 145 : 16
16 Waufumbua mkono wako, Wakishibisha kila kilicho hai matakwa yake.
Zaburi 25 : 5
5 Uniongoze katika kweli yako, Na kunifundisha. Maana Wewe ndiwe Mungu wa wokovu wangu, Nakungoja Wewe mchana kutwa.
Zaburi 145 : 1 – 232
1 Ee Mungu wangu, Mfalme, nitakutukuza, Nitalihimidi jina lako milele na milele.
2 Kila siku nitakuhimidi, Nitalisifu jina lako milele na milele.
3 BWANA ndiye mkuu mwenye kusifiwa sana, Wala ukuu wake hauchunguziki.
4 Kizazi kwa kizazi kitayasifu matendo yako, Kitayatangaza matendo yako makuu.
5 Nitaifikiri fahari ya utukufu wa adhama yako, Na matendo yako yote ya ajabu.
6 Watu watayataja matendo yako ya kutisha, Nami nitausimulia ukuu wako.
7 Watasimulia juu ya ukuu wa wema wako mwingi. Na wataiimba haki yako kwa sauti.
8 ⑩ BWANA ni mwenye fadhili na huruma, Si mwepesi wa hasira, ni mwingi wa rehema,
9 ⑪ BWANA ni mwema kwa watu wote, Na rehema zake ziko juu ya vyote alivyoumba.[25]
10 ⑫ Ee BWANA, kazi zako zote zitakushukuru, Na wacha Mungu wako watakuhimidi.
11 Wataunena utukufu wa ufalme wako, Na kusena uweza wako.
12 Ili kuwajulisha watu matendo yake makuu, Na utukufu wa fahari ya ufalme wake.
13 Ufalme wako ni ufalme wa milele, BWANA ni mwaminifu katika maneno yake yote, Na mwenye fadhili katika matendo yake yote[26] Na mamlaka yako ni ya vizazi vyote.
14 BWANA huwategemeza wote waangukao, Huwainua wote walioinama chini.
15 Macho ya watu wote yakuelekea Wewe, Nawe huwapa chakula chao wakati wake.
16 Waufumbua mkono wako, Wakishibisha kila kilicho hai matakwa yake.
17 BWANA ni mwenye haki katika njia zake zote, Na mwenye huruma katika matendo yake yote.
18 ⑬ BWANA yuko karibu na wote wamwitao, Wote wamwitao kwa uaminifu.
19 ⑭ Hutimiza matakwa ya wote wamchao, Na pia husikia kilio chao, na huwaokoa.
20 ⑮ BWANA huwahifadhi wote wampendao, Na wote wasio haki atawaangamiza.
21 Kinywa changu kitazinena sifa za BWANA; Wote wenye mwili na walihimidi jina lake takatifu milele na milele.
Leave a Reply