Biblia inasema nini kuhusu kushuhudia – Mistari yote ya Biblia kuhusu kushuhudia

Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia kushuhudia

Zaburi 66 : 16
16 Njoni, sikieni, ninyi nyote mnaomcha Mungu, Nami nitayatangaza aliyonitendea roho yangu.

Zaburi 40 : 9 – 10
9 ⑲ Nimehubiri habari za haki katika kusanyiko kubwa. Sikuizuia midomo yangu; Ee BWANA, unajua.
10 ⑳ Sikusitiri haki yako moyoni mwangu; Nimetangaza uaminifu wako na wokovu wako. Sikuficha fadhili zako wala kweli yako Katika kusanyiko kubwa.

Zaburi 107 : 1 – 2
1 ⑥ Mshukuruni BWANA kwa kuwa ni mwema, Kwa maana fadhili zake ni za milele.
2 Na waseme hivi waliokombolewa na BWANA, Wale aliowakomboa na mkono wa mtesi.

Warumi 10 : 17
17 Basi imani, hutokana na kusikia; na kusikia huja kwa neno la Kristo.

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *