Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia kusaidiwa kujiua
1 Wakorintho 6 : 19 – 20
19 ⑲ Au hamjui ya kuwa mwili wenu ni hekalu la Roho Mtakatifu aliye ndani yenu, mliyepewa na Mungu? Wala ninyi si mali yenu wenyewe;
20 ⑳ maana mlinunuliwa kwa thamani. Sasa basi, mtukuzeni Mungu katika miili yenu.
Kutoka 20 : 13
13 Usiue.
2 Wakorintho 12 : 9 – 10
9 Naye akaniambia, Neema yangu yakutosha; maana uweza wangu hutimilika katika udhaifu. Basi nitajisifia udhaifu wangu kwa furaha nyingi, ili uweza wa Kristo ukae juu yangu.
10 Kwa hiyo napendezwa na udhaifu, na matusi, na matatizo, na adha, na shida, kwa ajili ya Kristo. Maana niwapo dhaifu ndipo nilipo na nguvu.
Zaburi 34 : 17 – 20
17 Walilia, naye BWANA akasikia, Akawaponya kutoka kwa taabu zao zote.
18 BWANA yu karibu nao waliovunjika moyo, Na huwaokoa waliopondeka roho.
19 Mateso ya mwenye haki ni mengi, Lakini BWANA kutoka kwayo yote.
20 ⑫ Huihifadhi mifupa yake yote, Usivunjike hata mmoja.
1 Samweli 31 : 4 – 5
4 Ndipo Sauli akamwambia yule mchukua silaha zake, Futa upanga wako, unichome nao; wasije watu hawa wasiotahiriwa wakanichoma, na kunisimanga. Lakini huyo mchukua silaha zake akakataa; kwa sababu aliogopa sana. Basi Sauli akautwaa upanga wake, akauangukia.
5 Na mchukua silaha zake alipoona ya kuwa Sauli amekufa, yeye naye akauangukia upanga wake, akafa pamoja naye.
Leave a Reply