Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia kupanda mapema
Marko 1 : 35
35 Hata alfajiri na mapema sana akaondoka, akatoka akaenda zake mahali pasipokuwa na watu, akaomba huko.
Zaburi 119 : 148
148 ⑭ Nakaa macho usiku kucha, Ili kuitafakari ahadi yako.
Luka 1 : 78
78 ⑮ Kwa njia ya rehema za Mungu wetu, Ambazo kwa hizo mwangaza utokao juu umetufikia,
Zaburi 42 : 8
8 Mchana BWANA ataagiza fadhili zake, na usiku wimbo wake utakuwa nami, Naam, maombi kwa Mungu aliye uhai wangu.
1 Wathesalonike 5 : 5
5 Kwa kuwa ninyi nyote mmekuwa wana wa nuru, na wana wa mchana; sisi si wa usiku, wala wa giza.
Kutoka 34 : 4
4 Naye akachonga mbao mbili za mawe mfano wa zile za kwanza; na Musa akainuka na mapema asubuhi, naye akakwea katika mlima wa Sinai, kama BWANA alivyomwamuru, akazichukua hizo mbao mbili za mawe mkononi mwake.
Matendo 5 : 21
21 Nao waliposikia wakaenda alfajiri hekaluni, wakaanza kufundisha. Akaja Kuhani Mkuu nao waliokuwa pamoja naye, wakawakutanisha watu wa baraza, na wazee wote wa wana wa Israeli, wakatuma watu gerezani ili wawalete.
Marko 16 : 2
2 Na alfajiri mapema, siku ya kwanza ya juma, wakaenda kaburini, jua lilipoanza kuchomoza;
Luka 24 : 1
1 ⑮ Siku ya kwanza ya juma, ilipoanza kupambazuka, walikwenda kaburini, wakiyaleta manukato waliyoweka tayari.
Luka 4 : 40
40 Na jua lilipokuwa likichwa, wote waliokuwa na wagonjwa wenye maradhi mbalimbali waliwaleta kwake, akaweka mikono yake juu ya kila mmoja akawaponya.
Mhubiri 2 : 13
13 Ndipo nilipoona ya kuwa kweli hekima hupita upumbavu, kwa kadiri nuru ipitavyo giza;
Leave a Reply