Biblia inasema nini kuhusu kuongezeka – Mistari yote ya Biblia kuhusu kuongezeka

Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia kuongezeka

Isaya 54 : 2
2 Panua mahali pa hema yako, na wayatandaze mapazia ya maskani yako; usiwakataze; ongeza urefu wa kamba zako; vikaze vigingi vya hema yako.

2 Wakorintho 9 : 10
10 Na yeye ampaye mbegu mwenye kupanda, na mkate uwe chakula, atawapa mbegu za kupanda na kuzizidisha, naye atayaongeza mazao ya haki yenu;

Luka 6 : 38
38 Wapeni watu vitu, nanyi mtapewa; kipimo cha kujaa na kushindiliwa, na kusukwasukwa hata kumwagika, ndicho watu watakachowapa vifuani mwenu. Kwa kuwa kipimo kile kile mpimacho ndicho mtakachopimiwa.

1 Mambo ya Nyakati 4 : 9 – 10
9 Naye Yabesi alikuwa mwenye heshima kuliko nduguze; na mamaye akamwita Yabesi, akisema, Ni kwa sababu nilimzaa kwa huzuni.
10 Huyo Yabesi akamlingana Mungu wa Israeli, akisema, Lau kwamba ungenibariki kweli kweli, na kuipanua mipaka yangu, na mkono wako ukawa pamoja nami, nawe ungenilinda nisipatwe na maovu wala madhara! Naye Mungu akamjalia hayo aliyoyaomba.

Zaburi 115 : 14 – 15
14 BWANA na awaongeze ninyi, Ninyi na watoto wenu.
15 Na mbarikiwe ninyi na BWANA, Aliyezifanya mbingu na nchi.

Malaki 3 : 10
10 ③ Leteni zaka kamili ghalani, ili kiwemo chakula katika nyumba yangu, mkanijaribu kwa njia hiyo, asema BWANA wa majeshi; mjue kama sitawafungulia madirisha ya mbinguni, na kuwamwagieni baraka, hata isiwepo nafasi ya kutosha, au la.

Zaburi 119 : 32
32 Nitakwenda mbio katika njia ya maagizo yako, Utakaponipanulia ufahamu wangu.

Mithali 19 : 17
17 Amhurumiaye maskini humkopesha BWANA; Naye atamlipa kwa tendo lake jema.

Marko 4 : 24
24 Akawaambia, Angalieni msikialo; kipimo kile mpimacho ndicho mtakachopimiwa, na tena mtazidishiwa.

Warumi 13 : 8 – 10
8 ③ Msiwiwe na mtu chochote, isipokuwa kupendana; kwa maana ampendaye mwenzake ameitimiza sheria.
9 ④ Maana kule kusema, Usizini, Usiue, Usiibe, Usitamani; na ikiwapo amri nyingine yoyote, inajumlishwa katika neno hili, ya kwamba, Mpende jirani yako kama nafsi yako.
10 ⑤ Pendo halimfanyii jirani neno baya; basi pendo ndilo utimilifu wa sheria.

Kumbukumbu la Torati 1 : 11
11 BWANA, Mungu wa baba zenu, na awafanye kuwa wengi mara elfu kuliko mlivyo, na kuwabariki, kama alivyowaahidi.

Zaburi 18 : 36
36 Umezipanulia nafasi hatua zangu, Na miguu yangu haikuteleza.

Mwanzo 26 : 12
12 Mwaka huo Isaka akapanda mbegu katika nchi ile, naye akapata mavuno mara mia zaidi. BWANA akambariki.

Kumbukumbu la Torati 12 : 18 – 20
18 ⑤ lakini hivyo mtakula mbele za BWANA, Mungu wako, mahali atakapochagua BWANA, Mungu wako, wewe, na mwanao wa kiume na wa kike, na mtumwa wako mume na mke, na Mlawi aliye ndani ya malango yako; nawe furahi mbele za BWANA, Mungu wako, katika yote utakayotia mkono wako.
19 ⑥ Jilinde nafsi yako usimpuuze Mlawi siku zote utakazoishi katika nchi yako.
20 ⑦ BWANA, Mungu wako, atakapoongeza mpaka wako, kama alivyokuahidi, nawe utakaposema, Nataka kula nyama, kwa kuwa roho yako yatamani kula nyama; waweza kula nyama, kwa kufuata yote inayotamani roho yako.

Kutoka 34 : 24
24 Kwa kuwa mimi nitazitupa nje taifa za watu mbele yako, na kuipanua mipaka yako; wala hapana mtu yeyote atakayeitamani nchi yako, hapo utakapokwea kwenda kuhudhuria mbele za BWANA Mungu wako mara tatu kila mwaka.

2 Samweli 22 : 37
37 Umezifanyia nafasi hatua zangu, Wala miguu yangu haikuteleza.

Mathayo 25 : 26 – 30
26 Bwana wake akajibu, akamwambia, Wewe mtumwa mbaya na mlegevu, ulijua ya kuwa navuna nisipopanda, nakusanya nisipotawanya;
27 basi, ilikupasa kuiweka fedha yangu kwa watoao riba; nami nikija ningalipata iliyo yangu na faida yake.
28 Basi, mnyang’anyeni talanta hiyo, mpeni yule aliye nazo talanta kumi.
29 Kwa maana kila mwenye kitu atapewa, na kuongezewa tele; lakini asiye na kitu, hata kile alicho nacho atanyang’anywa.
30 Na mtumwa yule asiyefaa, mtupeni mbali katika giza la nje; ndiko kutakuwako kilio na kusaga meno.

Mwanzo 9 : 27
27 ⑥ Mungu amwongezee Yafethi. Na akae katika hema za Shemu; Na Kanaani awe mtumwa wake.

Isaya 65 : 24
24 Na itakuwa ya kwamba, kabla hawajaomba, nitajibu; na wakiwa bado wanena, nitasikia.

Kumbukumbu la Torati 19 : 1 – 232

1 BWANA, Mungu wako, atakapoyakatilia mbali hayo mataifa yenye nchi akupayo BWANA, Mungu wako, nawe ukawafuata, na kukaa katika miji yao, na katika nyumba zao;
2 itenge miji mitatu iwe kwako katikati ya nchi yako, akupayo BWANA, Mungu wako, kuimiliki.
3 Itengeze njia, igawanye na mipaka ya nchi yako, akurithishayo BWANA, Mungu wako, iwe mafungu matatu, ili kwamba kila mwenye kuua mtu apate kukimbilia huko.
4 Na hii ndiyo hukumu ya mwenye kuua mtu, atakayekimbilia huko awe hai; atakayemwua mwenziwe pasipo kukusudia, wala hakumchukia tangu hapo;
5 kama aingiapo mtu na mwenziwe mwituni kwenda kukata kuni, akapeleka mkono wake na shoka ili kukata mti, likatoka shoka katika mpini, likampiga yule mwenziwe hata akafa; basi na akimbilie katika miji hii mmojawapo awe hai;
6 asije akaandamiwa mwuaji na mwenye kulipiza kisasi cha damu, moyo wake ukali na hasira, akampata kwa njia kuwa ndefu, akamwua; wala hana haki ya kuuawa, kwa kuwa hakumchukia tangu hapo.
7 Kwa sababu hii ninakuamuru, na kukuambia, Ujitengee miji mitatu.
8 Na kama BWANA, Mungu wako, akiueneza mpaka wako kama alivyowaapia baba zako, akakupa na nchi yote aliyoahidi kwamba atawapa baba zako;
9 nawe ukiyashika maagizo haya yote nikuagizayo leo, na kuyafanya, kumpenda BWANA, Mungu wako, na kwenda sikuzote katika njia zake, ndipo ujiongezee miji mitatu tena, pamoja na mitatu ile;
10 isije ikamwagika damu ya asiye makosa kati ya nchi yako akupayo BWANA, Mungu wako, iwe urithi, ikawa na damu juu yako.
11 Lakini mtu awaye yote akimchukia mwenziwe na kumwotea na kumwinukia, akampiga hata akafa; naye akakimbilia miji hii mmojawapo;
12 ndipo wazee wa mji wake wapeleke ujumbe kumtwaa huko, na kumwua katika mkono wa mwenye kulipiza kisasi cha damu, apate kufa.
13 Jicho lako lisimhurumie, lakini uondoe damu ya asiye makosa katika Israeli, ili upate kufanikiwa.
14 Usiiondoe alama ya mpaka wa jirani yako, waliouweka watu wa kale katika urithi wako, utakaorithi ndani ya nchi akupayo BWANA, Mungu wako, uimiliki.
15 Shahidi mmoja asimwinukie mtu awaye yote kumshuhudia kwa uovu wowote, wala kwa dhambi yoyote, katika makosa akosayo yoyote; jambo na lithibitishwe kwa vinywa vya mashahidi wawili, au watatu.
16 Shahidi mdhalimu akimwinukia mtu yeyote na kushuhudia juu yake ya upotoe;
17 ndipo wale watu washindanao kwa mambo yale na wasimame wote wawili mbele za BWANA, mbele ya makuhani na waamuzi watakaokuwapo siku hizo;
18 nao waamuzi na watafute kwa bidii; na tazama, yule shahidi akiwa shahidi wa uongo, naye ametoa ushahidi wa uongo juu ya nduguye;
19 ndipo mtamfanyia kama alivyodhani kumfanyia nduguye; ndivyo utakavyoondoa uovu katikati yako.
20 Na watakaosalia watasikia na kuogopa, wasifanye tena uovu mfano wa huo katikati yako.
21 Wala jicho lako lisiwe na huruma; uzima kwa uzima, jicho kwa jicho, jino kwa jino, mkono kwa mkono, mguu kwa mguu.

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *