Biblia inasema nini kuhusu Kunyunyizia – Mistari yote ya Biblia kuhusu Kunyunyizia

Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Kunyunyizia

Mambo ya Walawi 14 : 7
7 ③ kisha atamnyunyizia huyo atakayetakaswa na ukoma mara saba, naye atasema kwamba ni safi, kisha atamwacha yule ndege aliye hai aende zake nyikani.

Mambo ya Walawi 14 : 51
51 kisha atatwaa huo mti wa mwerezi, na hisopo, na sufu nyekundu, pamoja na huyo ndege aliye hai, na kuvichovya vyote katika damu ya huyo ndege aliyechinjwa, na katika hayo maji ya mtoni, na kuinyunyizia nyumba mara saba;

Mambo ya Walawi 16 : 14
14 ⑩ Kisha atatwaa baadhi ya damu ya yule ng’ombe, na kuinyunyiza kwa kidole chake juu ya kiti cha rehema upande wa mashariki; na mbele ya kiti cha rehema atainyunyiza ile damu kwa kidole chake mara saba.

Waraka kwa Waebrania 9 : 13
13 Kwa maana, ikiwa damu ya mbuzi na mafahali na majivu ya ndama ya ng’ombe waliyonyunyiziwa wenye uchafu hutakasa hata kuusafisha mwili;

Waraka kwa Waebrania 9 : 19
19 Maana kila amri ilipokwisha kunenwa na Musa kwa hao watu wote, kama ilivyoamuru sheria, aliitwaa damu ya ndama na ya mbuzi, pamoja na maji na sufu nyekundu na hisopo, akakinyunyizia kitabu chenyewe, na watu wote,

Waraka kwa Waebrania 9 : 21
21 Na ile hema nayo na vyombo vyote vya ibada alivinyunyizia damu vivyo hivyo.

Waraka kwa Waebrania 11 : 28
28 ② Kwa imani akaifanya Pasaka, na kule kunyunyiza damu, ili yule mwenye kuwaangamiza wazaliwa wa kwanza asiwaguse wao.

Waraka kwa Waebrania 12 : 24
24 na Yesu mjumbe wa agano jipya, na damu ya kunyunyizwa, inenayo mema kuliko ile ya Habili.

Hesabu 8 : 7
7 ⑫ Nawe utawafanyia mambo haya ili kuwatakasa; nyunyiza juu yao maji yatakasayo dhambi, nao wajinyoe kwa wembe mwili wote, kisha wazifue nguo zao, na kujitakasa.

Ezekieli 36 : 25
25 Nami nitawanyunyizia maji safi, nanyi mtakuwa safi; nitawatakaseni kutoka kwa uchafu wenu wote, na kutoka kwa vinyago vyenu vyote.

Waraka kwa Waebrania 9 : 19
19 Maana kila amri ilipokwisha kunenwa na Musa kwa hao watu wote, kama ilivyoamuru sheria, aliitwaa damu ya ndama na ya mbuzi, pamoja na maji na sufu nyekundu na hisopo, akakinyunyizia kitabu chenyewe, na watu wote,

Waraka kwa Waebrania 10 : 22
22 ⑧ na tukaribie wenye moyo wa kweli, kwa utimilifu wa imani, hali tumenyunyiziwa mioyo tuache dhamiri mbaya, tumeoshwa miili kwa maji safi.

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *