Biblia inasema nini kuhusu kununua nyumba – Mistari yote ya Biblia kuhusu kununua nyumba

Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia kununua nyumba

Kumbukumbu la Torati 28 : 8
8 BWANA ataiamuru baraka ije juu yako katika ghala zako, na mambo yote utakayotia mkono wako; naye atakubarikia katika nchi akupayo BWANA, Mungu wako.

Mithali 24 : 27
27 Tengeneza kazi yako huko nje, Jifanyizie kazi yako tayari shambani, Ukiisha, jenga nyumba yako.

Yeremia 29 : 5
5 Jengeni nyumba, mkakae ndani yake, kapandeni bustani, mkale matunda yake;

Yoshua 1 : 3
3 Kila mahali zitakapopakanyaga nyayo za miguu yenu, nimewapa ninyi, kama nilivyomwapia Musa.

Kumbukumbu la Torati 11 : 31
31 Kwani ninyi mtavuka Yordani mwingie kuimiliki nchi awapayo BWANA, Mungu wenu, nanyi muimiliki na kuketi humo.

Mithali 24 : 3 – 4
3 Nyumba hujengwa kwa hekima, Na kwa ufahamu huthibitika,
4 Na kwa maarifa vyumba vyake hujazwa Vitu vyote vya thamani na vya kupendeza.

Kumbukumbu la Torati 6 : 9 – 11
9 Tena yaandike juu ya miimo ya nyumba yako, na juu ya malango yako.
10 Kisha BWANA Mungu wako atakapokuleta katika nchi aliyowaapia babu zako, Abrahamu na Isaka na Yakobo, ya kuwa atakupa; miji mikubwa mizuri usiyoijenga wewe,
11 na nyumba zimejaa vitu vyema vyote usizojaza wewe, na visima vilivyochimbwa usivyochimba wewe, mashamba ya mizabibu na mizeituni usiyoipanda wewe, nawe utakula na kushiba;

Kumbukumbu la Torati 15 : 6
6 ① Kwani BWANA, Mungu wako, atakubarikia, kama alivyokuahidi; nawe utakopesha mataifa mengi, lakini hutakopa; tena utayatawala mataifa mengi, usitawaliwe na wao.

Kumbukumbu la Torati 8 : 18
18 ⑳ Bali utamkumbuka BWANA, Mungu wako, maana ndiye akupaye nguvu za kupata utajiri; ili alifanye imara agano lake alilowapa baba zako, kama hivi leo.

Kumbukumbu la Torati 5 : 33
33 ⑳ Endeni njia yote aliyowaagiza BWANA, Mungu wenu, mpate kuwa hai, na kufanikiwa, mkafanye siku zenu kuwa nyingi katika nchi mtakayoimiliki.

Mithali 22 : 7
7 Tajiri humtawala maskini, Naye akopaye ni mtumwa wake akopeshaye.

Mithali 23 : 1 – 35
1 Utakapoketi kwa chakula pamoja na mtawala, Mwangalie sana yeye aliye mbele yako.
2 Tena ujitie kisu kooni, Kama ukiwa mlafi.
3 Usivitamani vyakula vyake vya anasa; Kwa maana ni vyakula vya hila.
4 Usijitaabishe ili kupata utajiri; Acha kuzitegemea akili zako mwenyewe.
5 Je! Utavikazia macho vile ambavyo si kitu? Maana bila shaka mali hujifanyia mabawa, Kama tai arukaye mbinguni.
6 Usile mkate wa mtu mwenye husuda; Wala usivitamani vyakula vyake vya anasa;
7 Maana aonavyo nafsini mwake, ndivyo alivyo. Akuambia, Haya, kula, kunywa; Lakini moyo wake hauwi pamoja nawe.
8 Tonge lile ulilokula utalitapika, Na maneno yako matamu yatakupotea.
9 Usiseme masikioni mwa mpumbavu; Maana atadharau hekima ya maneno yako.
10 Usiiondoe alama ya mpaka wa zamani; Wala usiingie katika mashamba ya yatima;
11 Kwa sababu mkombozi wao ana nguvu; Atawatetea juu yako.
12 Elekeza moyo wako kusikiliza mafundisho; Tega masikio yako kusikia maneno ya maarifa.
13 Usimnyime mtoto wako mapigo; Maana ukimpiga kwa fimbo hatakufa.
14 Utampiga kwa fimbo, Na kumwokoa nafsi yake na Kuzimu.
15 Mwanangu, kama moyo wako una hekima, Moyo wangu utafurahi, naam, moyo wangu;
16 Naam, viuno vyangu vitafurahi, Midomo yako inenapo maneno mema.
17 Moyo wako usiwahusudu wenye dhambi; Bali mche BWANA mchana kutwa;
18 Maana bila shaka iko thawabu; Na tumaini lako halitabatilika.
19 Sikia, mwanangu, uwe na hekima, Na kuuongoza moyo wako katika njia njema.
20 Usiwe miongoni mwao wanywao mvinyo; Miongoni mwao walao nyama kwa pupa.
21 Kwa maana mlevi na mlafi huingia umaskini, Na utepetevu humvika mtu nguo mbovu.
22 Msikilize baba yako aliyekuzaa, Wala usimdharau mama yako akiwa mzee.
23 Inunue kweli, wala usiiuze; Naam, hekima, na mafundisho, na ufahamu.
24 Baba yake mwenye haki atashangilia; Naye amzaaye mtoto mwenye hekima atamfurahia.
25 Na wafurahi baba yako na mama yako; Na afurahi aliyekuzaa.
26 Mwanangu, nipe moyo wako; Macho yako yapendezwe na njia zangu.
27 Kwa maana kahaba ni shimo refu; Na malaya ni mtego wa shimo jembamba.
28 Naam, huotea kama mnyang’anyi; Huwaongeza wenye hila katika wanadamu.
29 Ni nani apigaye, Yowe? Ni nani aliaye, Ole? Ni nani mwenye ugomvi? Ni nani mwenye mguno? Ni nani aliye na majeraha yasiyo na sababu? Ni nani aliye na macho mekundu?
30 Ni wale wakaao sana kwenye mvinyo; Waendao kutafuta divai iliyochanganyika.
31 Usiutazame mvinyo iwapo ni mwekundu; uitiapo bilauri rangi yake, ushukapo taratibu;
32 Mwisho wake huuma kama nyoka; Huchoma kama fira.
33 Macho yako yataona mambo mageni; Na moyo wako utatoa yaliyopotoka.
34 Naam, utakuwa kama alalaye katikati ya bahari; Au kama yeye asinziaye juu ya mlingoti.
35 Utasema, Wamenichapa wala sikuumia; Wamenipiga wala sina habari; Nitaamka lini, nitazidi kuitafuta tena.

Mwanzo 12 : 1 – 3
1 BWANA akamwambia Abramu, Toka wewe katika nchi yako, na jamaa zako, na nyumba ya baba yako, uende mpaka nchi nitakayokuonesha;
2 nami nitakufanya wewe kuwa taifa kubwa, na kukubariki, na kulikuza jina lako; nawe uwe baraka;
3 nami nitawabariki wakubarikio, naye akulaaniye nitamlaani; na katika wewe jamaa zote za dunia watabarikiwa.

Yoshua 1 : 11
11 Piteni katika kambi, mkawaamuru hao watu, mkisema, Tayarisheni vyakula; kwa maana baada ya siku tatu mtavuka mto huu wa Yordani, ili kuingia na kuimiliki nchi awapayo BWANA, Mungu wenu, mpate kuimiliki.

Isaya 32 : 18
18 Na watu wangu watakaa katika makao ya amani; na katika maskani zilizo salama, na katika mahali pa kupumzikia penye utulivu.

Yoshua 24 : 13
13 ⑫ Nami nimewapa ninyi nchi msiyoitendea kazi, na miji msiyoijenga, nanyi mmekaa humo; mnakula matunda ya mashamba ya mizabibu na mizeituni msiyoipanda.

Yeremia 29 : 11
11 Maana nayajua mawazo ninayowawazia ninyi, asema BWANA, ni mawazo ya amani wala si ya mabaya, kuwapa ninyi tumaini siku zenu za baadaye.

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *