kulinda moyo wako

Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia kulinda moyo wako

Mithali 4 : 23
23 Linda moyo wako kuliko yote uyalindayo; Maana ndiko zitokako chemchemi za uzima.

Wafilipi 4 : 6 – 7
6 Msijisumbue kwa neno lolote; bali katika kila neno kwa kusali na kuomba, pamoja na kushukuru, haja zenu na zijulikane na Mungu.
7 Na amani ya Mungu, ipitayo akili zote, itawahifadhi mioyo yenu na nia zenu katika Kristo Yesu.

Warumi 12 : 2
2 Wala msifuate kanuni za dunia hii; bali mgeuzwe kwa kufanywa upya nia zenu, mpate kujua hakika mapenzi ya Mungu yaliyo mema, ya kumpendeza, na ukamilifu.

Zaburi 73 : 26
26 Mwili wangu na moyo wangu hupunguka, Bali Mungu ni mwamba wa moyo wangu Na sehemu yangu milele.

Zaburi 51 : 10
10 ④ Ee Mungu, uniumbie moyo safi, Uifanye upya na kuithibiti roho yangu.

Wakolosai 3 : 5
5 Basi, viueni viungo vyenu vilivyo vya kidunia, uasherati, uchafu, tamaa mbaya, mawazo mabaya, na kutamani, ndiyo ibada ya sanamu;

Luka 6 : 45
45 Mtu mwema katika hazina njema ya moyo wake hutoa yaliyo mema, na mtu mwovu katika hazina mbovu ya moyo wake hutoa yaliyo maovu; kwa kuwa mtu, kinywa chake hunena yale yaujazayo moyo wake.

Mithali 23 : 26
26 Mwanangu, nipe moyo wako; Macho yako yapendezwe na njia zangu.

Mithali 4 : 1 – 27
1 Wanangu, yasikilizeni mausia ya baba yenu, Tegeni masikio mpate kujua ufahamu.
2 Kwa kuwa nawapa mafundisho mazuri; Msiiache sheria yangu.
3 Maana nilikuwa mwana kwa baba yangu, Mpole, mpenzi wa pekee wa mama yangu.
4 Naye akanifundisha, akaniambia, Moyo wako uyahifadhi maneno yangu; Shika amri zangu ukaishi.
5 Jipatie hekima, jipatie ufahamu; usiusahau; Wala usiyakatae maneno ya kinywa changu.
6 Usimwache, naye atakusitiri; Umpende, naye atakulinda.
7 Bora hekima, basi jipatie hekima; Naam, kwa mapato yako yote jipatie ufahamu.
8 Umtukuze, naye atakukuza; Atakupatia heshima, ukimkumbatia.
9 Atakupa neema kuwa kilemba kichwani; Na kukukirimia taji la uzuri.
10 Mwanangu, sikiliza, na kuzipokea kauli zangu; Na miaka ya maisha yako itakuwa mingi.
11 Nimekufundisha katika njia ya hekima; Nimekuongoza katika mapito ya unyofu.
12 Uendapo, hatua zako hazitadhiikika, Wala ukipiga mbio hutajikwaa.
13 Mkamate sana elimu, usimwache aende zake; Mshike, maana yeye ni uzima wako.
14 Usiingie katika njia ya waovu, Wala usitembee katika njia ya wabaya.
15 Jiepushe nayo, usipite karibu nayo, Igeukie mbali, ukaende zako.
16 Maana hawalali isipokuwa wametenda madhara; Huondolewa usingizi, ikiwa hawakumwangusha mtu.
17 Maana wao hula mkate wa uovu, Nao hunywa divai ya ujeuri.
18 Bali njia ya wenye haki ni kama nuru ing’aayo, Ikizidi kung’aa hata mchana mkamilifu.
19 Njia ya waovu ni kama giza; Hawajui ni kitu gani kiwakwazacho.
20 Mwanangu, sikiliza maneno yangu; Tega sikio lako, uzisikie kauli zangu.
21 Zisiondoke machoni pako; Uzihifadhi ndani ya moyo wako.
22 Maana ni uhai kwa wale wazipatao, Na afya ya mwili wao wote.
23 Linda moyo wako kuliko yote uyalindayo; Maana ndiko zitokako chemchemi za uzima.
24 Jiepushe na kinywa cha ujeuri, Na midomo ya upotovu uiweke mbali nawe.
25 Macho yako yatazame mbele, Na kope zako zitazame mbele yako sawasawa.
26 Ulisawazishe pito la mguu wako, Na njia zako zote zithibitike;
27 Usigeuke kwa kulia wala kwa kushoto; Ondoa mguu wako maovuni.

Mathayo 7 : 6
6 ⑭ Msiwape mbwa kilicho kitakatifu, wala msitupe lulu zenu mbele ya nguruwe, wasije wakazikanyaga chini ya miguu yao, wakageuka na kuwararua.

Wakolosai 3 : 1
1 Basi mkiwa mmefufuliwa pamoja na Kristo, yatafuteni yaliyo juu Kristo aliko, ameketi katika mkono wa kulia wa Mungu.

Mithali 7 : 25
25 Moyo wako usizielekee njia zake, Wala usipotee katika mapito yake.

1 Yohana 1 : 8
8 Tukisema kwamba hatuna dhambi, tunajidanganya wenyewe, wala kweli haimo ndani yetu.

Yohana 10 : 10
10 Mwizi huja tu kuiba, kuua na kuharibu; mimi nilikuja ili wawe na uzima, tena wawe nao tele.

Yoshua 1 : 8
8 Kitabu hiki cha torati kisiondoke kinywani mwako, bali yatafakari maneno yake mchana na usiku, upate kuangalia kutenda kulingana na maneno yote yaliyoandikwa humo; maana ndipo utakapoifanikisha njia yako, kisha ndipo utakapositawi sana.

Warumi 3 : 10
10 kama ilivyoandikwa, ya kwamba, Hakuna mwenye haki hata mmoja.

1 Samweli 2 : 9
9 Yeye atailinda miguu ya watakatifu wake; Bali waovu watanyamazishwa gizani, Maana kwa nguvu hakuna atakayeshinda;

1 Wathesalonike 4 : 1 – 8
1 ⑦ Iliyobaki, ndugu, tunawasihi na kuwaonya kwamba mwenende katika Bwana Yesu; kama mlivyopokea kwetu jinsi iwapasavyo kuenenda na kumpendeza Mungu, kama nanyi mnavyoenenda, vivyo hivyo mpate kuzidi sana.
2 Kwa kuwa mnajua ni maagizo gani tuliyowapa kwa Bwana Yesu.
3 ⑧ Maana haya ndiyo mapenzi ya Mungu, kutakaswa kwenu, mwepukane na uasherati;
4 ⑩ kila mmoja wenu ajue kuuweza mwili wake katika utakatifu na heshima;
5 ⑪ si katika hali ya tamaa mbaya, kama Mataifa wasiomjua Mungu.
6 ⑫ Mtu asimpunje ndugu yake wala kumkosea katika jambo hili; kwa sababu Bwana ndiye alipizaye kisasi cha haya yote; kama tulivyowaambia kwanza, tukashuhudia sana.
7 ⑬ Maana Mungu hakutuitia uchafu, bali tuwe katika utakaso.
8 ⑭ Basi yeye anayekataa, hakatai mwanadamu bali Mungu, anayewapa ninyi Roho wake Mtakatifu.

Wagalatia 5 : 24
24 ⑰ Na hao walio wa Kristo Yesu wameusulubisha mwili pamoja na mawazo yake mabaya na tamaa zake.

Warumi 10 : 17
17 Basi imani, hutokana na kusikia; na kusikia huja kwa neno la Kristo.

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *