Biblia inasema nini kuhusu Kujinyima – Mistari yote ya Biblia kuhusu Kujinyima

Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Kujinyima

Mwanzo 22 : 12
12 Akasema, Usimnyoshee kijana mkono wako, wala usimtendee neno; kwa maana sasa ninajua ya kuwa unamcha Mungu, kwa kuwa hukunizuilia mwanao, mwanao wa pekee.

2 Samweli 24 : 24
24 ⑩ Lakini mfalme akamwambia Arauna, La, sivyo; lakini kweli nitavinunua kwako kwa thamani yake; wala sitamtolea BWANA, Mungu wangu, sadaka za kuteketezwa isiyonigharimu chochote. Hivyo Daudi akakinunua hicho kiwanja cha kupuria na wale ng’ombe kwa shekeli hamsini za fedha.

Zaburi 132 : 5
5 Hadi nitakapompatia BWANA mahali, Na Mwenye nguvu wa Yakobo maskani”.

Mithali 16 : 32
32 Asiye mwepesi wa hasira ni mwema kuliko shujaa; Na mtu aitawalaye roho yake kuliko mtu atekaye mji.

Mithali 23 : 2
2 Tena ujitie kisu kooni, Kama ukiwa mlafi.

Danieli 10 : 3
3 Sikula chakula kitamu, wala nyama wala divai haikuingia kinywani mwangu, wala sikujipaka mafuta kabisa, hata majuma matatu kamili yalipotimia.

Mathayo 5 : 30
30 ⑱ Na mkono wako wa kulia ukikukosesha, ukate uutupe mbali nawe; kwa maana yakufaa kiungo chako kimoja kipotee kuliko mwili wako wote kutupwa katika Jehanamu.

Marko 9 : 43
43 Na mkono wako ukikukosesha, ukate; ni afadhali kuingia katika uzima ukiwa kibutu, kuliko kuwa na mikono miwili, na kwenda zako Jehanamu, kwenye moto usiozimika; [

Mathayo 8 : 22
22 ① Lakini Yesu akamwambia, Nifuate; waache wafu wazike wafu wao.

Luka 9 : 60
60 Akamwambia Waache wafu wawazike wafu wao; bali wewe nenda ukautangaze ufalme wa Mungu.

Mathayo 10 : 39
39 ⑬ Mwenye kuiona nafsi yake ataipoteza; naye mwenye kuipoteza nafsi yake kwa ajili yangu ataiona.

Mathayo 13 : 46
46 ⑧ naye alipoona lulu moja ya thamani kubwa, alikwenda akauza alivyo navyo vyote, akainunua.

Mathayo 16 : 25
25 Kwa kuwa mtu atakaye kuiokoa nafsi yake, ataipoteza; na mtu atakayepoteza nafsi yake kwa ajili yangu, ataiona.

Marko 8 : 35
35 ⑰ Kwa kuwa mtu atakaye kuiponya nafsi yake, ataiangamiza, na mtu atakayeiangamiza nafsi yake kwa ajili yangu na kwa ajili ya Injili, huyu ataisalimisha.

Luka 9 : 24
24 ③ Kwa kuwa mtu atakaye kuiponya nafsi yake ataiangamiza, na mtu atakayeiangamiza nafsi yake kwa ajili yangu ndiye atakayeisalimisha.

Mathayo 18 : 9
9 Na jicho lako likikukosesha, ling’oe, ukalitupe mbali nawe; ni afadhali kuingia katika uzima ukiwa na chongo, kuliko kuwa na macho mawili, na kutupwa katika Jehanamu ya moto.

Mathayo 19 : 12
12 Maana wako matowashi waliozaliwa hali hiyo toka matumboni mwa mama zao; tena wako matowashi waliofanywa na watu kuwa matowashi; tena wako matowashi waliojifanya kuwa matowashi kwa ajili ya ufalme wa mbinguni. Awezaye kulipokea neno hili, na alipokee.

Mathayo 19 : 21
21 Yesu akamwambia, Ukitaka kuwa mkamilifu, nenda ukauze ulivyo navyo, uwape maskini, nawe utakuwa na hazina mbinguni; kisha njoo unifuate.

Luka 12 : 33
33 ④ Viuzeni mlivyo navyo, mtoe sadaka. Jifanyieni mifuko isiyochakaa, akiba isiyopungua katika mbingu, mahali pasipokaribia mwizi, wala nondo haharibu. ⑤

Luka 5 : 11
11 ② Hata walipokwisha kuziegesha mashua zao pwani, wakaacha vyote wakamfuata.

Luka 5 : 27
27 ⑧ Baada ya hayo akatoka, akaona mtoza ushuru, jina lake Lawi, ameketi forodhani, akamwambia, Nifuate.

Marko 2 : 14
14 ④ Na alipokuwa akipita, akamwona Lawi wa Alfayo, ameketi forodhani, akamwambia, Nifuate. Akaondoka akamfuata.

Luka 14 : 33
33 Basi, kadhalika kila mmoja wenu asiyeacha vyote alivyo navyo, hawezi kuwa mwanafunzi wangu.

Luka 18 : 30
30 asiyepokea zaidi mara nyingi katika wakati huu, na katika ulimwengu ujao uzima wa milele.

Marko 10 : 29
29 Yesu akasema, Amin, nawaambieni, Hakuna mtu aliyeacha nyumba, au ndugu wa kiume, au ndugu wa kike, au mama, au baba, au watoto, au mashamba, kwa ajili yangu, na kwa ajili ya Injili,

Luka 21 : 4
4 maana, hao wote walitoa sadaka katika mali iliyowazidi, bali huyu katika umaskini wake ametia vyote alivyokuwa navyo.

Marko 12 : 44
44 ⑳ maana hao wote walitia baadhi ya mali iliyowazidi; bali huyu katika umaskini wake ametia vyote alivyokuwa navyo, ndiyo riziki yake yote pia.

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *