Biblia inasema nini kuhusu kujiamini – Mistari yote ya Biblia kuhusu kujiamini

Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia kujiamini

Wafilipi 4 : 13
13 Nayaweza mambo yote katika yeye anitiaye nguvu.

Wafilipi 1 : 6
6 Nami niliaminilo ndilo hili, ya kwamba yeye aliyeanza kazi njema mioyoni mwenu ataimaliza hata siku ya Kristo Yesu;

Yuda 1 : 24
24 Yeye awezaye kuwalinda ninyi msijikwae, na kuwasimamisha mbele ya utukufu wake bila mawaa katika furaha kuu;

Wafilipi 3 : 10
10 ⑳ ili nimjue yeye, na uweza wa kufufuka kwake, na ushirika wa mateso yake, nikifananishwa na kufa kwake;

2 Timotheo 1 : 12
12 Kwa sababu hiyo nimepatikana na mateso haya, lakini sitahayari; kwa maana namjua yeye niliyemwamini, na kusadiki ya kwamba aweza kukilinda kile nilichokiweka amana kwake hata siku ile.

Yohana 15 : 7
7 Ninyi mkikaa ndani yangu, na maneno yangu yakikaa ndani yenu, ombeni lolote mtakalo nanyi mtatendewa.

Marko 11 : 23
23 Amin, nawaambia, yeyote atakayeuambia mlima huu, Ng’oka ukatupwe baharini, wala asione shaka moyoni mwake, ila aamini kwamba hayo asemayo yametukia, yatakuwa yake.

2 Wakorintho 5 : 17
17 Hata imekuwa, mtu akiwa ndani ya Kristo amekuwa kiumbe kipya; ya kale yamepita, tazama! Yamekuwa mapya.

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *