kuitwa na Mungu

Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia kuitwa na Mungu

Mathayo 22 : 14
14 Kwa maana waitwao ni wengi, bali wateule ni wachache.

Yeremia 33 : 3
3 ⑯ Niite, nami nitakuitikia, nami nitakuonesha mambo makubwa, magumu usiyoyajua.

Yohana 6 : 44
44 Hakuna mtu awezaye kuja kwangu, asipovutwa na Baba aliyenituma; nami nitamfufua siku ya mwisho.

2 Timotheo 1 : 9
9 ambaye alituokoa akatuita kwa mwito mtakatifu, si kwa kadiri ya matendo yetu sisi, bali kwa kadiri ya makusudi yake mwenyewe na neema yake. Neema hiyo tulipewa katika Kristo Yesu kabla ya wakati kuanza,

Wafilipi 1 : 6
6 Nami niliaminilo ndilo hili, ya kwamba yeye aliyeanza kazi njema mioyoni mwenu ataimaliza hata siku ya Kristo Yesu;

Zaburi 138 : 8
8 ⑯ BWANA atanitimizia malengo yake kwangu; Ee BWANA, fadhili zako ni za milele; Usiiache kazi ya mikono yako.

Waraka kwa Waebrania 10 : 25
25 ⑫ wala tusiache kukusanyika pamoja, kama ilivyo desturi ya wengine; bali tuonyane; na kuzidi kufanya hivyo, kwa kadiri muonavyo siku ile kuwa inakaribia.

Luka 12 : 32
32 ③ Msiogope, enyi kundi dogo; kwa kuwa Baba yenu ameona vema kuwapa ule ufalme.

Warumi 8 : 28 – 30
28 Nasi twajua ya kuwa katika mambo yote Mungu hufanya kazi pamoja na wale wampendao katika kuwapatia mema, yaani, wale walioitwa kwa kusudi lake.
29 Maana wale aliowajua tangu asili, aliwachagua tangu asili wafananishwe na mfano wa Mwana wake, ili yeye awe mzaliwa wa kwanza miongoni mwa ndugu wengi.
30 Na wale aliowachagua tangu asili, hao akawaita; na wale aliowaita, hao akawahesabia haki; na wale aliowahesabia haki, hao akawatukuza.

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *