Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Kuhesabiwa haki
Mwanzo 15 : 6
6 Akamwamini BWANA, naye akamhesabia jambo hili kuwa haki.
Warumi 4 : 3
3 Maana Maandiko yasemaje? Abrahamu alimwamini Mungu, ikahesabiwa kwake kuwa haki.
Zaburi 32 : 2
2 Heri ambaye BWANA hamhesabii hatia, Na ambaye rohoni mwake hamna hila.
Zaburi 71 : 16
16 ⑪ Nitakuja na mambo ya ajabu ya Bwana MUNGU; Nitawakumbusha watu haki yako Wewe peke yako.
Zaburi 89 : 16
16 Kwa jina lako hufurahi mchana kutwa, Na kwa haki yako hutukuzwa.
Isaya 42 : 21
21 BWANA akapendezwa, kwa ajili ya haki yake, kuitukuza sheria, na kuiadhimisha.
Isaya 45 : 25
25 Katika BWANA wazao wote wa Israeli watapewa haki, na kutukuka.
Isaya 46 : 13
13 Mimi ninaleta karibu haki yangu, haitakuwa mbali, na wokovu wangu hautakawia; nami nitaweka wokovu katika Sayuni kwa ajili ya Israeli, utukufu wangu.
Isaya 50 : 8
8 ④ Yeye anipatiaye haki yangu yu karibu; ni nani atakayeshindana nami? Na tusimame pamoja; ni nani aliye hasimu yangu? Na anikaribie basi.
Isaya 51 : 6
6 ⑬ Inueni macho yenu mbinguni, mkaitazame nchi chini; maana mbingu zitatoweka kama moshi, na nchi itachakaa kama vazi, nao wakaao ndani yake watakufa kadhalika; bali wokovu wangu utakuwa wa milele, na ukombozi wangu hautakoma kamwe.
Isaya 53 : 11
11 ③ Ataona mazao ya taabu ya nafsi yake, na kuridhika. Kwa maarifa yake mtumishi wangu mwenye haki Atawafanya wengi kuwa wenye haki; Naye atayachukua maovu yao.
Isaya 54 : 17
17 ⑭ Kila silaha itengenezwayo juu yako haitafanikiwa, na kila ulimi utakaoinuka juu yako katika hukumu utauhukumu kuwa mkosa. Huu ndio urithi wa watumishi wa BWANA, na haki yao inayotoka kwangu mimi, asema BWANA.
Isaya 56 : 1
1 BWANA asema hivi, Shikeni hukumu, mkatende haki; kwa maana wokovu wangu uko karibu kuja, na haki yangu kufunuliwa.
Isaya 61 : 10
10 Nitafurahi sana katika BWANA, nafsi yangu itashangilia katika Mungu wangu; maana amenivika mavazi ya wokovu, amenifunika vazi la haki, kama bwana arusi ajipambavyo kwa kilemba cha maua, na kama bibi arusi ajipambavyo kwa vyombo vya dhahabu.
Yeremia 23 : 6
6 Katika siku zake Yuda ataokolewa, na Israeli atakaa salama, na jina lake atakaloitwa ni hili, BWANA ni haki yetu.
Zekaria 3 : 4
4 ③ Naye malaika akajibu, akawaambia wale waliosimama mbele yake, akisema, Mvueni nguo hizi chafu. Kisha akamwambia yeye, Tazama, nimekuondolea uovu wako, nami nitakuvika mavazi ya thamani kubwa.
Yohana 5 : 24
24 ⑦ Amin, amin, nawaambia, Yeye alisikiaye neno langu na kumwamini yeye aliyenituma ana uzima wa milele; wala haingii hukumuni, bali amepita kutoka mautini kuingia uzimani.
Matendo 13 : 39
39 na kwa yeye kila amwaminiye huhesabiwa haki katika mambo yale yote asiyoweza kuhesabiwa haki kwa Torati ya Musa.
Warumi 1 : 17
17 Kwa maana haki ya Mungu inadhihirishwa ndani yake, toka imani hadi imani; kama ilivyoandikwa, Mwenye haki ataishi kwa imani.
Habakuki 2 : 4
4 Tazama, roho yake hujivuna, haina unyofu ndani yake; lakini mwenye haki ataishi kwa imani yake.
Wagalatia 3 : 11
11 ⑦ Ni dhahiri ya kwamba hakuna mtu ahesabiwaye haki mbele za Mungu katika sheria; kwa sababu Mwenye haki ataishi kwa imani.
Warumi 2 : 13
13 ④ Kwa sababu sio wale waisikiao sheria walio wenye haki mbele za Mungu, bali ni wale waitendao sheria watakaohesabiwa haki.
Warumi 3 : 22
22 ni haki ya Mungu iliyo kwa njia ya imani katika Yesu Kristo kwa wote waaminio. Maana hakuna tofauti;
Warumi 3 : 26
26 apate kuonesha haki yake wakati huu, ili awe mwenye haki na mwenye kumhesabia haki yeye amwaminiye Yesu.
Warumi 3 : 28
28 Basi, twaona ya kuwa mwanadamu huhesabiwa haki kwa imani pasipo matendo ya sheria.
Warumi 3 : 30
30 kama kwa kweli Mungu ni mmoja, atakayewahesabia haki wale waliotahiriwa katika imani, nao wale wasiotahiriwa atawahesabia haki kwa njia ya imani iyo hiyo.
Warumi 4 : 25
25 ⑭ ambaye alitolewa kwa ajili ya makosa yetu, na kufufuliwa ili mpate kuhesabiwa haki.
Warumi 5 : 1
1 ⑮ Basi tukiisha kuhesabiwa haki itokayo katika imani, na muwe na amani kwa Mungu, kwa njia ya Bwana wetu Yesu Kristo,
Leave a Reply