Biblia inasema nini kuhusu kufuru – Mistari yote ya Biblia kuhusu kufuru

Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia kufuru

Mathayo 12 : 31 – 32
31 ⑱ Kwa sababu hiyo nawaambia, Kila dhambi na kila neno la kufuru watasamehewa wanadamu, ila kwa kumkufuru Roho hawatasamehewa.
32 ⑲ Naye mtu yeyote atakayenena neno juu ya Mwana wa Adamu atasamehewa, bali yeye atakayenena neno juu ya Roho Mtakatifu hatasamehewa katika ulimwengu wa sasa, wala katika ule ujao.

Waraka kwa Waebrania 10 : 29
29 ⑯ Mwaonaje? Haikumpasa adhabu iliyo kubwa zaidi mtu yule aliyemkanyaga Mwana wa Mungu, na kuihesabu damu ya agano aliyotakaswa kwayo kuwa ni kitu ovyo, na kumfanyia jeuri Roho wa neema?

Luka 12 : 10
10 Na kila mtu atakayenena neno juu ya Mwana wa Mtu atasamehewa, bali aliyemkufuru Roho Mtakatifu hatasamehewa.

Marko 3 : 29
29 bali mtu atakayemkufuru Roho Mtakatifu hana msamaha hata milele; ila atakuwa ana dhambi ya milele,

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *