Biblia inasema nini kuhusu Kufunga – Mistari yote ya Biblia kuhusu Kufunga

Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Kufunga

2 Samweli 1 : 12
12 wakaomboleza, wakalia, wakafunga hadi jioni, kwa ajili ya Sauli, na kwa ajili ya Yonathani mwanawe, na kwa ajili ya watu wa BWANA na kwa ajili ya nyumba ya Israeli; kwa sababu wameanguka kwa upanga.

Zaburi 35 : 13
13 Bali mimi, walipougua wao, Nguo yangu ilikuwa gunia. Nilijitesa nafsi yangu kwa kufunga; Maombi yangu yakarejea kifuani mwangu.

Danieli 6 : 18
18 Kisha mfalme akaenda nyumbani kwake, akakesha usiku kucha, akafunga; na vinanda havikuletwa mbele yake; na usingizi wake ukampaa.

2 Samweli 12 : 16
16 ④ Basi Daudi akamwomba Mungu kwa ajili ya mtoto; Daudi akafunga, akaingia, akalala chini usiku kucha.

Esta 4 : 16
16 ⑬ Nenda ukawakusanye Wayahudi wote waliopo hapa Susa, mkafunge kwa ajili yangu; msile wala kunywa muda wa siku tatu, usiku wala mchana, nami na wajakazi wangu tutafunga vile vile; kisha nitaingia kwa mfalme, kinyume cha sheria; nami nikiangamia, na niangamie.

Matendo 13 : 3
3 ④ Ndipo wakiisha kufunga na kuomba, wakaweka mikono yao juu yao, wakawaacha waende zao.

Matendo 14 : 23
23 ⑫ Na walipokwisha kuwachagulia wazee katika kila kanisa, na kuomba pamoja na kufunga, wakawaweka katika mikono ya Bwana waliyemwamini.

Danieli 9 : 3
3 Nikamwelekezea Bwana Mungu uso wangu, ili kusihi kwa maombi, na dua, pamoja na kufunga, na kuvaa nguo za magunia na majivu.

1 Samweli 7 : 6
6 ⑯ Wakakusanyika huko Mispa, wakateka maji na kuyamimina mbele za BWANA; wakafunga siku ile, wakasema huko, Tumemfanyia BWANA dhambi. Samweli akawaamua wana wa Israeli huko Mispa.

Nehemia 9 : 2
2 Waliokuwa wa wazao wa Israeli wakajitenga na wageni wote, wakasimama, wakaziungama dhambi zao, na maovu ya baba zao.

Kumbukumbu la Torati 9 : 18
18 Nikaanguka chini mbele za BWANA siku arubaini usiku na mchana, kama pale kwanza; sikula chakula wala kunywa maji; kwa sababu ya makosa yenu yote mliyofanya, kwa kufanya yaliyo maovu machoni pa BWANA, kwa kumkasirisha.

Nehemia 9 : 1
1 Hata siku ya ishirini na nne ya mwezi huo wana wa Israeli wakawa wamekusanyika, wakifunga, wenye kuvaa magunia, na kujitia udongo vichwani.[14]

Kumbukumbu la Torati 9 : 9
9 Na hapo nilipokwea mlimani kwenda kuzipokea mbao za mawe, nazo ni mbao za agano BWANA alilofanya nanyi, ndipo nikakaa mle mlimani siku arubaini usiku na mchana; sikula chakula wala kunywa maji.

Kumbukumbu la Torati 9 : 18
18 Nikaanguka chini mbele za BWANA siku arubaini usiku na mchana, kama pale kwanza; sikula chakula wala kunywa maji; kwa sababu ya makosa yenu yote mliyofanya, kwa kufanya yaliyo maovu machoni pa BWANA, kwa kumkasirisha.

Mathayo 4 : 2
2 ⑰ Akafunga siku arubaini mchana na usiku, mwishowe akaona njaa.

Marko 1 : 13
13 Akawako huko jangwani siku arubaini, hali akijaribiwa na Shetani; naye alikuwa pamoja na wanyama wa mwituni, na malaika walikuwa wakimhudumia.

Luka 4 : 2
2 akijaribiwa na Ibilisi. Na siku hizo alikuwa hali kitu; na zilipotimia, aliona njaa.

Mathayo 9 : 14
14 ⑮ Wakati ule wanafunzi wake Yohana wakamwendea, wakasema, Kwa nini sisi na Mafarisayo tunafunga, bali wanafunzi wako hawafungi?⑯

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *