Biblia inasema nini kuhusu kufundisha – Mistari yote ya Biblia kuhusu kufundisha

Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia kufundisha

2 Timotheo 3 : 16 – 17
16 Kila andiko, lenye pumzi ya Mungu, lafaa kwa mafundisho, na kwa kuwaonya watu makosa yao, na kwa kuwaongoza, na kwa kuwaadibisha katika haki;
17 ili mtu wa Mungu awe kamili, amekamilishwa apate kutenda kila tendo jema.

2 Timotheo 2 : 23 – 26
23 ⑤ Lakini uyakatae maswali ya upumbavu yasiyo na elimu, ukijua ya kuwa huzaa magomvi.
24 ⑥ Tena haimpasi mtumwa wa Bwana kuwa mgomvi; bali kuwa mwanana kwa watu wote, awezaye kufundisha, mvumilivu;
25 ⑦ akiwaonya kwa upole wao washindanao naye, ili kama ikiwezekana, Mungu awajalie ili watubu na kuijua kweli;
26 wapate tena fahamu zao, na kutoka katika mtego wa Ibilisi, ambaye amewanasa, hata wakayafanya mapenzi yake.

Yakobo 3 : 1
1 ⑫ Ndugu zangu, msiwe waalimu wengi, mkijua ya kuwa mtapata hukumu kubwa zaidi.

2 Timotheo 4 : 2
2 lihubiri neno, uwe tayari, wakati ukufaao na wakati usiokufaa, karipia, kemea, na kuonya kwa uvumilivu wote na mafundisho.

Kumbukumbu la Torati 6 : 4 – 9
4 Sikiliza, Ee Israeli; BWANA, Mungu wetu, BWANA ndiye mmoja[3]
5 Nawe mpende BWANA, Mungu wako, kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa nguvu zako zote.
6 Na maneno haya ninayokuamuru leo, yatakuwa katika moyo wako;
7 nawe uwafundishe watoto wako kwa bidii, na kuyasema uishipo katika nyumba yako, na utembeapo njiani, na ulalapo, na uondokapo.
8 Yafunge yawe dalili juu ya mkono wako, nayo yatakuwa kama utepe katikati ya macho yako.
9 Tena yaandike juu ya miimo ya nyumba yako, na juu ya malango yako.

1 Timotheo 4 : 13
13 Hata nitakapokuja, ufanye bidii katika kusoma Maandiko, kuonya na kufundisha.

Waefeso 6 : 7
7 kwa nia njema kama kumtumikia Bwana wala si mwanadamu;

Waefeso 6 : 4
4 ② Nanyi, akina baba, msiwachokoze watoto wenu; bali waleeni katika adabu na maagizo ya Bwana.

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *