Biblia inasema nini kuhusu kufanya kazi siku ya sabato – Mistari yote ya Biblia kuhusu kufanya kazi siku ya sabato

Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia kufanya kazi siku ya sabato

Kutoka 35 : 2
2 Fanyeni kazi siku sita, lakini siku ya saba itakuwa siku takatifu kwenu; ni Sabato ya kustarehe kabisa kwa BWANA; mtu yeyote atakayefanya kazi yoyote katika siku hiyo atauawa.

Mathayo 12 : 11 – 12
11 ④ Akawaambia, Ni mtu yupi miongoni mwenu mwenye kondoo mmoja, na yule kondoo ametumbukia shimoni siku ya sabato, asiyemshika akamwopoa?
12 ⑤ Je! Mtu ni bora kuliko kondoo mara ngapi? Basi ni halali kutenda mema siku ya sabato.

Kutoka 20 : 10
10 lakini siku ya saba ni Sabato ya BWANA, Mungu wako, siku hiyo usifanye kazi yoyote, wewe, wala mwana wako, wala binti yako, wala mtumwa wako, wala mjakazi wako, wala mnyama wako wa kufuga, wala mgeni aliye ndani ya malango yako.

Yohana 5 : 18
18 ② Basi kwa sababu hiyo Wayahudi walizidi kutaka kumwua, kwa kuwa hakuivunja sabato tu, bali pamoja na hayo alimwita Mungu Baba yake, akijifanya sawa na Mungu. Basi Yesu akajibu, akawaambia, Amin, amin, nawaambia,

Wakolosai 2 : 16
16 ⑱ Basi, mtu asiwahukumu ninyi katika vyakula au vinywaji, au kwa sababu ya sikukuu au mwandamo wa mwezi, au sabato;

Kutoka 35 : 3
3 Hamtawasha moto katika nyumba zenu kwa siku ya Sabato.

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *