Biblia inasema nini kuhusu kuchoka – Mistari yote ya Biblia kuhusu kuchoka

Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia kuchoka

Mithali 19 : 15
15 Uvivu humtia mtu katika usingizi mzito; Na nafsi yake mvivu itaona njaa.

Mhubiri 2 : 24 – 26
24 ② Mwanadamu hapati jema kupita kula na kunywa, na kuiburudisha roho yake kwa mema katika kazi yake. Hayo nayo niliona ya kwamba hutoka mkononi mwa Mungu.
25 Kwa maana ni nani awezaye kula au kujiburudisha kuliko mimi?
26 ③ Kwa sababu Mungu humpa yeye aliyemridhia hekima na maarifa na furaha; bali mkosaji humpa taabu, ili kukusanya na kututa, apate kumpa huyo ambaye Mungu amridhia. Hayo nayo ni ubatili na kufukuza upepo.

2 Timotheo 2 : 22
22 ④ Lakini zikimbie tamaa za ujanani; ukafuate haki, na imani, na upendo, na amani, pamoja na wale wamwitao Bwana kwa moyo safi.

2 Timotheo 2 : 15
15 Jitahidi kujionesha kuwa umekubaliwa na Mungu, mfanyakazi asiye na sababu ya kutahayari, ukitumia kwa halali neno la kweli.

Mhubiri 9 : 10
10 Lolote mkono wako utakalolipata kulifanya, ulifanye kwa nguvu zako; kwa kuwa hakuna kazi, wala shauri, wala maarifa, wala hekima, huko kuzimu uendako wewe.

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *