Biblia inasema nini kuhusu kucheza – Mistari yote ya Biblia kuhusu kucheza

Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia kucheza

Zaburi 149 : 3
3 Na walisifu jina lake kwa kucheza, Kwa sauti tamu ya matari na kinubi.

Zaburi 150 : 4
4 Msifuni kwa matari na kucheza; Msifuni kwa zeze na filimbi;

Mhubiri 3 : 4
4 ⑦ Wakati wa kulia, na wakati wa kucheka; Wakati wa kuomboleza, na wakati wa kucheza;

Zaburi 30 : 11
11 ⑱ Umegeuza msiba wangu kuwa ngoma; Umeniondolea huzuni yangu, kunijalia furaha tele.

Yeremia 31 : 13
13 Ndipo bikira atafurahi katika kucheza, na vijana na wazee pamoja; maana nitageuza masikitiko yao kuwa furaha, nami nitawafariji, na kuwafurahisha waache huzuni zao.

Kutoka 32 : 19
19 Hata alipokaribia kambini akaiona ile ndama, na ile michezo. Hasira ya Musa ikawaka, akazitupa zile mbao mikononi mwake, akazivunja chini ya mlima.

Zaburi 150 : 1 – 6
1 Haleluya. Msifuni Mungu katika patakatifu pake; Msifuni katika anga la uweza wake.
2 Msifuni kwa matendo yake makuu; Msifuni kwa kadiri ya wingi wa ukuu wake.
3 Msifuni kwa mvumo wa baragumu; Msifuni kwa kinanda na kinubi;
4 Msifuni kwa matari na kucheza; Msifuni kwa zeze na filimbi;
5 Msifuni kwa matoazi yaliayo; Msifuni kwa matoazi yavumayo sana.
6 ① Kila mwenye pumzi na amsifu BWANA. Haleluya.

Kutoka 15 : 20
20 Na Miriamu, nabii mwanamke, dada yake Haruni, akatwaa tari mkononi mwake; wanawake wakatoka wote wakaenda nyuma yake, wenye matari na kucheza.

Waamuzi 11 : 34
34 ⑦ Kisha Yeftha akafika Mispa nyumbani kwake, na tazama, binti yake akamtokea kumlaki, na matari na akichezacheza; naye alikuwa ni mwanawe wa pekee; hakuwa na mwingine, wa kiume wala binti.

2 Samweli 6 : 16
16 Ikawa, sanduku la BWANA lilipoingia mji wa Daudi, Mikali binti Sauli, akachungulia dirishani, akamwona mfalme Daudi akirukaruka na kucheza mbele za BWANA; akamdharau moyoni mwake.

Luka 15 : 25
25 Basi, yule mwanawe mkubwa alikuwa shambani na alipokuwa akija na kuikaribia nyumba, alisikia sauti ya nyimbo na nderemo.

Mhubiri 3 : 1 – 4
1 ④ Kwa kila jambo kuna majira yake, Na wakati kwa kila kusudi chini ya mbingu.
2 ⑤ Wakati wa kuzaliwa, na wakati wa kufa; Wakati wa kupanda, na wakati wa kung’oa kilichopandwa;
3 ⑥ Wakati wa kuua, na wakati wa kuponya; Wakati wa kubomoa, na wakati wa kujenga;
4 ⑦ Wakati wa kulia, na wakati wa kucheka; Wakati wa kuomboleza, na wakati wa kucheza;

2 Samweli 6 : 14
14 ⑲ Daudi akacheza mbele za BWANA kwa nguvu zake zote; na Daudi alikuwa amevaa naivera ya kitani.

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *