Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia kubarikiwa
Waefeso 2 : 8
8 ③ Kwa maana mmeokolewa kwa neema, kwa njia ya imani; ambayo hiyo haikutokana na nafsi zenu, ni kipawa cha Mungu;
Zaburi 32 : 1
1 Heri aliyesamehewa dhambi, Na kuondolewa makosa yake.
Zaburi 1 : 1
1 Heri mtu yule asiyekwenda Katika shauri la wasio haki; Wala hakusimama katika njia ya wenye dhambi; Wala hakuketi barazani pa wenye mizaha.
Tito 3 : 5
5 ① si kwa sababu ya matendo ya haki tuliyoyatenda sisi; bali kwa rehema yake, kwa kuoshwa kwa kuzaliwa kwa mara ya pili na kufanywa upya na Roho Mtakatifu;
Yohana 3 : 16
16 Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele.
Zaburi 127 : 3
3 Tazama, watoto ni urithi kutoka kwa BWANA, Uzao wa tumbo ni thawabu.
Mathayo 5 : 1 – 12
1 Naye alipowaona makundi ya watu, alipanda mlimani; na alipokwisha kuketi, wanafunzi wake walimjia;
2 akafumbua kinywa chake, akawafundisha, akisema,
3 Heri walio maskini wa roho; Maana ufalme wa mbinguni ni wao.
4 Heri wenye huzuni; Maana hao watafarijika.
5 Heri wenye upole; Maana hao watairithi nchi.
6 Heri wenye njaa na kiu ya haki; Maana hao watashibishwa.
7 Heri wenye rehema; Maana hao watapata rehema.
8 Heri wenye moyo safi; Maana hao watamwona Mungu.
9 Heri wapatanishi; Maana hao wataitwa wana wa Mungu.
10 Heri wenye kuudhiwa kwa ajili ya haki; Maana ufalme wa mbinguni ni wao.
11 ① Heri ninyi watakapowashutumu na kuwaudhi na kuwanenea kila neno baya kwa uongo, kwa ajili yangu.
12 ② Furahini, na kushangilia; kwa kuwa thawabu yenu ni kubwa mbinguni; kwa maana ndivyo walivyowaudhi manabii waliokuwa kabla yenu.
Yohana 1 : 12
12 Bali wote waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu, ndio wale waliaminio jina lake;
Kumbukumbu la Torati 28 : 1 – 3
1 ⑳ Itakuwa utakaposikia sauti ya BWANA, Mungu wako, kwa bidii, kutunza kuyafanya maagizo yake yote nikuagizayo leo, ndipo BWANA, Mungu wako, atakapokutukuza juu ya mataifa yote ya duniani;
2 na baraka hizi zote zitakujilia na kukupata usikiapo sauti ya BWANA, Mungu wako.
3 Utabarikiwa mjini, utabarikiwa na mashambani.
Mwanzo 12 : 1 – 3
1 BWANA akamwambia Abramu, Toka wewe katika nchi yako, na jamaa zako, na nyumba ya baba yako, uende mpaka nchi nitakayokuonesha;
2 nami nitakufanya wewe kuwa taifa kubwa, na kukubariki, na kulikuza jina lako; nawe uwe baraka;
3 nami nitawabariki wakubarikio, naye akulaaniye nitamlaani; na katika wewe jamaa zote za dunia watabarikiwa.
Yakobo 4 : 7
7 Basi mtiini Mungu. Mpingeni Shetani, naye atawakimbia.
Wagalatia 3 : 28
28 Hakuna Myahudi wala Mgiriki. Hakuna mtumwa wala huru. Hakuna mwanamume wala mwanamke. Maana ninyi nyote mmekuwa wamoja katika Kristo Yesu.
Zaburi 146 : 5
5 ⑱ Heri ambaye Mungu wa Yakobo ni msaada wake, Na tumaini lake ni kwa BWANA, Mungu wake,
Zaburi 1 : 1 – 6
1 Heri mtu yule asiyekwenda Katika shauri la wasio haki; Wala hakusimama katika njia ya wenye dhambi; Wala hakuketi barazani pa wenye mizaha.
2 Bali sheria ya BWANA ndiyo impendezayo, Na sheria yake huitafakari mchana na usiku.
3 Naye atakuwa kama mti uliopandwa Kandokando ya vijito vya maji, Uzaao matunda yake kwa majira yake, Wala jani lake halinyauki; Na kila alitendalo litafanikiwa.
4 Sivyo walivyo wasio haki; Hao ni kama makapi yapeperushwayo na upepo.
5 Kwa hiyo wasio haki hawatasimama hukumuni, Wala wakosaji katika kusanyiko la wenye haki.
6 Kwa kuwa BWANA anaijua njia ya wenye haki, Bali njia ya wasio haki itapotea.
Leave a Reply