Biblia inasema nini kuhusu Komamanga – Mistari yote ya Biblia kuhusu Komamanga

Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Komamanga

1 Samweli 14 : 2
2 Naye Sauli alikuwa akikaa katika Viunga vya Gibea, chini ya mkomamanga uliokuwa kwenye uwanja huko Migroni; na hao watu waliokuwa pamoja naye walikuwa watu mia sita;

Hesabu 13 : 23
23 Wakafika bonde la Eshkoli, na huko wakakata tawi lenye kishada kimoja cha zabibu, wakalichukua kwa mti kati ya watu wawili; wakaleta makomamanga pia, na tini.

Kutoka 28 : 34
34 njuga ya dhahabu na komamanga, katika pindo za joho kuizunguka pande zote.

Kutoka 39 : 24
24 Nao wakatia katika upindo wa joho makomamanga ya nyuzi za rangi ya samawati, na rangi ya zambarau, na rangi nyekundu, na kitani iliyosokotwa.

1 Wafalme 7 : 18
18 Hivyo akazitengeneza nguzo; na kulikuwa na safu mbili za kuzunguka juu ya wavu mmoja, zifunike mataji yaliyokuwako juu ya vichwa vya nguzo; akafanya vivyo hivyo kwa taji la pili.

1 Wafalme 7 : 20
20 ⑦ Kulikuwako tena taji juu ya nguzo mbili, karibu na uvimbe uliokuwako kando ya wavu; na makomamanga yalikuwa mia mbili, safu safu pande zote juu ya taji la pili.

1 Wafalme 7 : 42
42 na makomamanga mia nne ya zile nyavu mbili; safu mbili za makomamanga kwa kila wavu, kuyafunika nayo mabakuli mawili ya mataji yaliyokuwa juu ya nguzo;

Yeremia 52 : 23
23 ⑬ Palikuwa na makomamanga tisini na sita katika pande zake; makomamanga; yote yalikuwa mia moja juu ya wavu huo pande zote.

Wimbo ulio Bora 8 : 2
2 Ningekuongoza nyumbani mwa mamangu, Naye angenifundisha;[3] Ningekunywesha divai iliyokolea, Divai mpya ya mkomamanga wangu.

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *