Biblia inasema nini kuhusu Kinu – Mistari yote ya Biblia kuhusu Kinu

Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Kinu

Yeremia 25 : 10
10 Tena, nitawaondolea sauti ya kicheko, na sauti ya furaha, sauti ya bwana arusi, na sauti ya bibi arusi, sauti ya mawe ya kusagia, na nuru ya mishumaa.

Kumbukumbu la Torati 24 : 6
6 ⑤ Mtu awaye yote asitwae jiwe la kusagia, la juu wala la chini, kuwa rehani; kwani hivi ni kutwaa maisha ya mtu kuwa rehani.

Ayubu 41 : 24
24 Moyo wake una uimara kama jiwe; Naam, uimara kama jiwe la chini la kusagia.

Isaya 47 : 2
2 Twaa mawe ya kusagia, usage unga; Vua utaji wako, ondoa mavazi yako, Funua mguu wako, pita katika mito ya maji.

Kutoka 11 : 5
5 na wazaliwa wa kwanza wote katika nchi ya Misri watakufa, tangu yule mzaliwa wa kwanza wa Farao aketiye katika kiti chake cha enzi, hata mzaliwa wa kwanza wa huyo kijakazi aliye pale nyuma ya jiwe la kusagia; na wazaliwa wa kwanza wote wa wanyama.

Mathayo 24 : 41
41 wanawake wawili watakuwa wakisaga; mmoja atwaliwa, mmoja aachwa.

Waamuzi 16 : 21
21 Wafilisti wakamkamata, wakamng’oa macho; wakateremka naye mpaka Gaza, wakamfunga kwa vifungo vya shaba; naye alikuwa akisaga ngano katika gereza.

Maombolezo 5 : 13
13 Vijana huyachukua mawe ya kusagia; Na watoto hujikwaa chini ya kuni.

Hesabu 11 : 8
8 Watu wakazungukazunguka na kuikusanya, kisha wakaisaga kwa mawe ya kusagia, au kuitwanga katika vinu, kisha wakaitokosa vyunguni na kuandaa mikate; na ladha yake ilikuwa kama ladha ya mafuta mapya.

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *