Kinara

Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Kinara

Kutoka 25 : 40
40 Nawe angalia ya kwamba uvifanye kama mfano wake, uliooneshwa mlimani.

Kutoka 37 : 24
24 Akakifanya cha talanta moja ya dhahabu safi, pamoja na vyombo vyake vyote.

Hesabu 8 : 4
4 ⑩ Na hii ndiyo kazi ya hicho kinara cha taa, ilikuwa ni kazi ya ufuzi wa dhahabu; tangu kitako chake hata maua yake kilikuwa ni kazi ya ufuzi; vile vile kama ule mfano BWANA aliokuwa amemwonesha Musa, ndivyo alivyokifanya kinara.

Kutoka 26 : 35
35 ⑩ Na ile meza utaiweka nje ya pazia, na kinara cha taa kuikabili ile meza upande wa maskani wa kuelekea kusini; na ile meza utaiweka upande wa kaskazini.

Kutoka 40 : 25
25 Kisha akaziwasha taa zake mbele za BWANA, kama BWANA alivyomwamuru Musa.

Waraka kwa Waebrania 9 : 2
2 Maana hema ilitengenezwa, ile ya kwanza, mlimokuwa na kinara cha taa, na meza, na mikate mitakatifu; ndipo palipoitwa, Patakatifu.

Kutoka 25 : 38
38 Na makoleo yake, na visahani vyake, vyote vitakuwa vya dhahabu safi.

Kutoka 37 : 23
23 Kisha akafanya taa zake saba, makoleo yake na visahani vyake, vya dhahabu safi.

Hesabu 4 : 10
10 nao watakitia, na vyombo vyake vyote, ndani ya ngozi ya pomboo,[7] na kukiweka juu ya miti ya kukichukulia

Kutoka 27 : 21
21 ⑳ Ndani ya ile hema ya kukutania, nje ya hilo pazia, lililo mbele ya huo ushuhuda, Haruni na wanawe wataitengeza tangu jioni hadi asubuhi mbele ya BWANA; itakuwa ni amri ya milele katika vizazi vyao vyote kwa ajili ya wana wa Israeli.

Kutoka 30 : 7
7 Na Haruni atafukiza uvumba wa manukato juu yake; kila siku asubuhi atakapozitengeneza zile taa, ataufukiza.

Hesabu 4 : 4
4 Huu ndio utumishi wa wana wa Kohathi katika hema ya kukutania, katika vile vyombo vitakatifu sana;

Hesabu 4 : 15
15 ⑥ Na Haruni na wanawe watakapokwisha kupafunika mahali patakatifu, na vyombo vyote vya mahali patakatifu, hapo watakapong’oa kambi; baadaye, wana wa Kohathi watakuja kuvichukua; lakini wasiviguse vile vitu vitakatifu, wasife. Vyombo vile ni mzigo wa wana wa Kohathi katika hema ya kukutania.

1 Samweli 3 : 3
3 ⑳ na taa ya Mungu ilikuwa haijazimika bado, na Samweli alikuwa amelala katika hekalu la BWANA, palipokuwa na sanduku la Mungu;

1 Wafalme 7 : 50
50 na vikombe, na makasi, na mabakuli, na miiko, na vyetezo, vya dhahabu safi; na bawaba za dhahabu, za milango ya nyumba ya ndani, yaani, patakatifu pa patakatifu, na za milango ya nyumba, ndiyo hekalu.

1 Mambo ya Nyakati 28 : 15
15 kwa uzani tena kwa vinara vya dhahabu, na kwa taa zake za dhahabu, kwa uzani, kwa kila kinara, na kwa taa zake; na kwa vinara vya fedha, kwa uzani kwa kila kinara na kwa taa zake, kwa kadiri ya matumizi ya kila kinara;

2 Mambo ya Nyakati 4 : 20
20 na vinara na taa zake, ziwake kama ilivyoagizwa mbele ya chumba cha ndani, vya dhahabu iliyosafika;

Yeremia 52 : 19
19 Navyo vikombe, na vyombo vya kutolea majivu, na mabakuli, na masufuria, na vinara, na miiko, na vyetezo, vilivyokuwa vya dhahabu katika dhahabu, na vilivyokuwa vya fedha katika fedha, kamanda wa askari walinzi akavichukua.

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *