Biblia inasema nini kuhusu kilemba – Mistari yote ya Biblia kuhusu kilemba

Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia kilemba

Kutoka 28 : 4
4 Na mavazi watakayoyafanya ni haya; kifuko cha kifuani, na naivera, na joho, na kanzu ya kazi ya urembo; na kilemba, na mshipi; nao watawafanyia Haruni nduguyo, na wanawe, mavazi matakatifu ili anitumikie katika kazi ya ukuhani.

Kutoka 28 : 39
39 Na hiyo kanzu utaifuma ya kitani nzuri ya kazi ya urembo, ufanye na kilemba cha nguo ya kitani nzuri, nawe utafanya mshipi wenye kunakishiwa vizuri.

Kutoka 39 : 31
31 Nao wakatia ukanda wa rangi ya samawati ili kulifunga katika hicho kilemba upande wa juu; vile vile kama BWANA alivyomwagiza Musa.

Ezekieli 21 : 26
26 Bwana MUNGU asema hivi; Kiondoe kilemba, livue taji; haya hayatakuwa tena kama yalivyo; kikweze kilicho chini, kakishushe kilichoinuka.

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *