Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Kayafa
Luka 3 : 2
2 wakati wa ukuhani mkuu wa Anasi na Kayafa, neno la Mungu lilimfikia Yohana, mwana wa Zakaria, jangwani.
Yohana 18 : 13
13 Wakampeleka kwa Anasi kwanza; maana alikuwa baba mkwe wa Kayafa, yule aliyekuwa Kuhani Mkuu mwaka ule.
Yohana 11 : 51
51 Na neno hilo yeye hakulisema kwa nafsi yake; bali kwa kuwa alikuwa Kuhani Mkuu mwaka ule, alitabiri ya kwamba Yesu atakufa kwa ajili ya taifa hilo.
Yohana 18 : 14
14 ⑫ Naye Kayafa ndiye yule aliyewapa Wayahudi lile shauri ya kwamba yafaa mtu mmoja afe kwa ajili ya watu.
Mathayo 26 : 3
3 Wakati ule wakuu wa makuhani, na wazee wa watu, wakakusanyika katika behewa ya Kuhani Mkuu, jina lake Kayafa;
Mathayo 26 : 57
57 Nao waliomkamata Yesu wakampeleka kwa Kayafa, Kuhani Mkuu, walikokuwa wamekutanika waandishi na wazee.
Mathayo 26 : 65
65 Ndipo Kuhani Mkuu akararua mavazi yake, akisema, Amekufuru; mna haja gani tena ya mashahidi? Tazameni, sasa mmesikia hiyo kufuru yake;
Yohana 18 : 24
24 Basi Anasi akampeleka akiwa amefungwa kwa Kayafa, Kuhani Mkuu.
Yohana 18 : 28
28 ⑯ Kisha wakamchukua Yesu kutoka kwa Kayafa mpaka Praitorio,[5] nayo ikawa alfajiri; lakini wao wenyewe hawakuingia ndani ya ile Praitorio, wasije wakanajisika, bali wapate kuila Pasaka.
Matendo 4 : 22
22 maana umri wake yule mtu aliyefanyiwa ishara hii ya kuponya ulipita miaka arubaini.
Leave a Reply