Biblia inasema nini kuhusu kashfa – Mistari yote ya Biblia kuhusu kashfa

Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia kashfa

Mathayo 12 : 36
36 Basi, nawaambia, Kila neno lisilo maana, watakalolinena wanadamu, watatoa hesabu ya neno hilo siku ya hukumu.

Mithali 10 : 18
18 Yeye afichaye chuki ana midomo ya uongo, Na yeye asingiziaye ni mpumbavu.

1 Petro 3 : 16
16 Nanyi muwe na dhamiri njema, ili katika neno lile mnalosingiziwa, watahayarishwe wale wautukanao mwenendo wenu mwema katika Kristo.

Zaburi 101 : 5
5 Amsingiziaye jirani yake kwa siri, Huyo nitamwangamiza. Mwenye macho ya kiburi na moyo wa majivuno, Huyo sitamvumilia.

Yakobo 4 : 11
11 Ndugu, msisingiziane; amsingiziaye ndugu yake, au kumhukumu ndugu yake, huisingizia sheria na kuihukumu sheria. Lakini ukiihukumu sheria, huwi mtenda sheria, bali umekuwa hakimu.

Mithali 16 : 28
28 Mtu mshupavu huleta fitina; Na mchongezi huwafarakanisha rafiki.

Tito 3 : 2
2 wasimtukane mtu yeyote, wasiwe wagomvi, wawe wema, wakiwa wapole sana kwa watu wote.

1 Petro 2 : 1
1 Basi, wekeni mbali uovu wote na hila yote, na unafiki na husuda na masingizio yote.

Kutoka 20 : 16
16 Usimshuhudie jirani yako uongo.

Luka 6 : 45
45 Mtu mwema katika hazina njema ya moyo wake hutoa yaliyo mema, na mtu mwovu katika hazina mbovu ya moyo wake hutoa yaliyo maovu; kwa kuwa mtu, kinywa chake hunena yale yaujazayo moyo wake.

Mathayo 7 : 12
12 ⑰ Basi yoyote myatakayo mtendewe na watu, nanyi watendeeni vivyo hivyo; maana hiyo ndiyo Torati na Manabii.

1 Wakorintho 4 : 13
13 tukisingiziwa twasihi; tumefanywa kama takataka za dunia, na kuwa duni ya vitu vyote hata sasa.

Mathayo 5 : 11
11 ① Heri ninyi watakapowashutumu na kuwaudhi na kuwanenea kila neno baya kwa uongo, kwa ajili yangu.

1 Petro 3 : 10
10 Kwa maana, Atakaye kupenda maisha, Na kuona siku njema, Auzuie ulimi wake usinene mabaya, Na midomo yake isiseme uongo.

Mithali 11 : 9
9 Asiyemcha Mungu humpoteza jirani yake kwa kinywa chake; Bali wenye haki watapona kwa maarifa.

Mithali 20 : 19
19 Mwenye udaku hufunua siri; Basi, usishirikiane naye afunuaye midomo yake sana.

Kutoka 23 : 1
1 Usivumishe habari za uongo; usishirikiane na mwovu kwa kuwa shahidi wa uongo.

Zaburi 109 : 3
3 Naam, kwa maneno ya chuki wamenizunguka, Wamepigana nami bure.

Waefeso 4 : 32
32 ⑱ tena iweni wafadhili ninyi kwa ninyi, wenye huruma, mkasameheane kama Mungu katika Kristo alivyowasamehe ninyi.

Marko 7 : 20 – 23
20 Akasema, Kimtokacho mtu ndicho kimtiacho unajisi.
21 Kwa maana ndani ya mioyo ya watu hutoka mawazo mabaya, uasherati,
22 wizi, uuaji, uzinzi, tamaa mbaya, ukorofi, hila, ufisadi, kijicho, matukano, kiburi, upumbavu.
23 Haya yote yaliyo maovu yatoka ndani, nayo yamtia mtu unajisi.

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *