Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia jina bure
Kutoka 20 : 7
7 ⑲ Usilitaje bure jina la BWANA, Mungu wako, maana BWANA hatamhesabia kuwa hana hatia mtu alitajaye jina lake bure.
Mambo ya Walawi 19 : 12
12 ⑯ Msiape uongo kwa jina langu, na ukalinajisi jina la Mungu wako; Mimi ndimi BWANA.
Ezekieli 39 : 7
7 Na jina langu takatifu nitalifanya kuwa limejulikana kati ya watu wangu Israeli; wala sitaliacha jina langu takatifu kutiwa unajisi tena; nao mataifa watajua ya kuwa mimi ndimi BWANA, na Aliye Mtakatifu katika Israeli.
Leave a Reply