Jesse

Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Jesse

Ruthu 4 : 17
17 Nao wale wanawake waliokuwa jirani zake wakampa jina, wakisema, Naomi amezaliwa mwana; wakamwita jina lake Obedi;[7] yeye ndiye baba yake Yese, aliye baba yake Daudi.

1 Samweli 17 : 12
12 Basi Daudi alikuwa mwana wa yule Mwefrata, wa Bethlehemu ya Yuda, aliyeitwa jina lake Yese; naye huyo alikuwa na wana wanane; na yeye mwenyewe alikuwa mzee siku za Sauli, na mkongwe miongoni mwa watu.

Mathayo 1 : 6
6 Yese akamzaa mfalme Daudi. Daudi akamzaa Sulemani kwa yule mke wa Uria;

1 Samweli 16 : 13
13 Ndipo Samweli akaitwaa pembe yenye mafuta, akamtia mafuta kati ya ndugu zake; na Roho ya BWANA ikamjia Daudi kwa nguvu kuanzia siku ile. Basi Samweli akaondoka, akaenda zake Rama.

1 Samweli 16 : 23
23 Ikawa, ile roho mbaya kutoka kwa Mungu ilipomjia Sauli, ndipo Daudi alipokishika kinubi na kukipiga kwa mkono wake, naye Sauli akaburudishwa, na ile roho mbaya ikamwacha.

1 Samweli 17 : 28
28 ⑥ Naye Eliabu, mkubwa wake, alisikia hapo alipoongea na watu; na hasira yake Eliabu ikawaka juu ya Daudi, akasema, Mbona wewe umeshuka hapa? Na kondoo wale wachache umemwachia nani kule nyikani? Mimi nakujua kiburi chako, na ubaya wa moyo wako; maana umeshuka ili upate kuvitazama vita.

1 Samweli 22 : 4
4 Akawaleta mbele ya mfalme wa Moabu, nao wakakaa pamoja naye wakati wote Daudi alipokuwa ngomeni.

1 Mambo ya Nyakati 2 : 17
17 ⑭ Na Abigaili akamzaa Amasa; na babaye Amasa ni Yetheri, Mwishmaeli.

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *