Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Jemadari
Marko 15 : 45
45 Hata alipokwisha kupata hakika kutoka kwa yule kamanda, alimpa Yusufu yule maiti.
Matendo 21 : 32
32 Mara akatwaa askari na maofisa, akawaendea mbio. Nao walipomwona jemadari na askari wakaacha kumpiga Paulo.
Matendo 22 : 26
26 Yule jemadari aliposikia, akaenda akamwarifu yule jemadari, akisema, Unataka kufanya nini? Kwa maana mtu huyu ni Mrumi.
Matendo 23 : 17
17 Paulo akamwita ofisa mmoja, akasema, Mchukue kijana huyu kwa jemadari; maana ana neno la kumwarifu.
Matendo 23 : 23
23 Akawaita maofisa wawili, akasema, Wekeni tayari askari mia mbili kwenda Kaisaria, na askari wapanda farasi sabini, na wenye mikuki mia mbili, kabla ya saa tatu usiku.
Matendo 24 : 23
23 ② Akamwamuru yule ofisa kwamba Paulo alindwe; ila awe na nafasi, wala asimkataze mmojawapo wa rafiki zake kumtumikia.
Mathayo 8 : 13
13 Naye Yesu akamwambia yule afisa, Nenda zako; na iwe kwako kama ulivyoamini. Mtumishi wake akapona wakati ule ule.
Luka 7 : 10
10 Na wale waliotumwa waliporudi nyumbani, wakamkuta yule mtumwa ni mzima.
Mathayo 27 : 54
54 Basi yule afisa, na hao waliokuwa pamoja naye wakimlinda Yesu, walipoliona tetemeko la ardhi na mambo yaliyofanyika, wakaogopa sana, wakisema, Hakika huyu alikuwa Mwana wa Mungu.
Marko 15 : 39
39 Basi yule kamanda, aliyesimama hapo akimwelekea, alipoona ya kuwa alikata roho jinsi hii, akasema, Hakika mtu huyu alikuwa Mwana wa Mungu.
Leave a Reply