Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Injili
Mathayo 4 : 23
23 Naye alikuwa akizunguka katika Galilaya yote, akifundisha katika masinagogi yao, na kuihubiri Habari Njema ya ufalme, na kuponya kila ugonjwa na maradhi ya kila namna waliyokuwa nayo watu.
Mathayo 24 : 14
14 Tena Habari Njema ya ufalme itahubiriwa katika ulimwengu wote, kuwa ushuhuda kwa mataifa yote; hapo ndipo ule mwisho utakapokuja.
Warumi 1 : 1
1 Paulo, mtumwa wa Kristo Yesu, aliyeitwa kuwa mtume, na kutengwa aihubiri Injili ya Mungu;
Warumi 15 : 16
16 ili niwe mhudumu wa Kristo Yesu kati ya watu wa Mataifa, niifanyie Injili ya Mungu kazi ya ukuhani, kusudi Mataifa wawe sadaka yenye kibali, ikiisha kutakaswa na Roho Mtakatifu.
1 Wathesalonike 2 : 8
8 Hivyo ndivyo nasi tukiwajali kwa upendo mwingi, tuliona furaha kuwapa, si Injili ya Mungu tu, bali na roho zetu pia, kwa sababu mmekuwa wapendwa wetu.
1 Timotheo 1 : 11
11 kama ilivyonenwa katika Habari Njema ya utukufu wa Mungu ahimidiwaye, niliyowekewa amana.
1 Petro 4 : 17
17 ⑧ Kwa maana wakati umefika wa hukumu kuanza katika nyumba ya Mungu; na ikianza kwetu sisi, mwisho wao wasioitii Injili ya Mungu utakuwaje?
Marko 1 : 1
1 Mwanzo wa Injili ya Yesu Kristo, Mwana wa Mungu.
Warumi 1 : 16
16 Kwa maana siionei haya Injili; kwa sababu ni uweza wa Mungu uuletao wokovu, kwa kila aaminiye, kwa Myahudi kwanza, na kwa Mgiriki pia.
1 Wakorintho 9 : 12
12 ⑧ Ikiwa wengine wanashiriki uwezo huu juu yenu, sisi si zaidi? Lakini hatukuutumia uwezo huo; bali twayavumilia mambo yote tusije tukaizuia Habari Njema ya Kristo.
1 Wakorintho 9 : 18
18 ⑮ Basi thawabu yangu ni nini? Ni hii, ya kuwa ninapohubiri, nitaitoa Injili bila gharama, bila kutumia kwa utimilifu uwezo wangu nilio nao katika Injili.
Wagalatia 1 : 7
7 Wala si nyingine; lakini wapo watu wawataabishao na kutaka kuigeuza Injili ya Kristo.
Wafilipi 1 : 27
27 Lakini mwenendo wenu na uwe kama inavyoipasa Injili ya Kristo, ili, nikija na kuwaona ninyi, au nisipokuwapo, niyasikie mambo yenu, kama mnasimama imara katika roho moja, kwa moyo mmoja mkiishindania imani ya Injili;
1 Wathesalonike 3 : 2
2 Tukamtuma Timotheo ndugu yetu, mtumishi wa Mungu katika Injili ya Kristo, ili kuwafanya ninyi imara na kuwafariji katika imani yenu;
Waefeso 3 : 2
2 ⑳ ikiwa mmesikia habari ya uwakili wa neema ya Mungu niliyopewa kwa ajili yenu;
Matendo 20 : 24
24 ⑱ Lakini siyahesabu maisha yangu kuwa kitu cha thamani kwangu kama kuumaliza mwendo wangu na huduma ile niliyopokea kwa Bwana Yesu, kuishuhudia Habari Njema ya neema ya Mungu.
Waefeso 1 : 13
13 Nanyi pia katika huyo mmekwisha kulisikia neno la kweli, Habari Njema za wokovu wenu; tena mmekwisha kumwamini yeye, na kutiwa mhuri na Roho yule wa ahadi aliye Mtakatifu.
Waefeso 6 : 15
15 ⑫ na kama viatu vilivyofungiwa miguuni mwenu muwe tayari kutangaza Injili ya amani;
Luka 16 : 16
16 Torati na Manabii vilikuwapo mpaka Yohana; tangu wakati huo Habari Njema ya ufalme wa Mungu hutangazwa, na kila mtu hujiingiza kwa nguvu.
Leave a Reply