Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia iliyoshinikizwa chini ikitikiswa pamoja
Luka 6 : 38
38 Wapeni watu vitu, nanyi mtapewa; kipimo cha kujaa na kushindiliwa, na kusukwasukwa hata kumwagika, ndicho watu watakachowapa vifuani mwenu. Kwa kuwa kipimo kile kile mpimacho ndicho mtakachopimiwa.
2 Wakorintho 9 : 6
6 Lakini nasema neno hili, Apandaye haba atavuna haba; apandaye kwa ukarimu atavuna kwa ukarimu.
Marko 11 : 24
24 Kwa sababu hiyo nawaambia, Yoyote myaombayo mkisali, aminini ya kwamba mnayapokea, nayo yatakuwa yenu.
Matendo 20 : 35
35 Katika mambo yote nimewaonesha ya kuwa kwa kushika kazi hivi imewapasa kuwasaidia wanyonge, na kuyakumbuka maneno ya Bwana Yesu, jinsi alivyosema mwenyewe, Ni heri kutoa kuliko kupokea.
Yakobo 4 : 3
3 Hata mwaomba, wala hampati kwa sababu mwaomba vibaya, ili mvitumie kwa tamaa zenu.
Yohana 15 : 7
7 Ninyi mkikaa ndani yangu, na maneno yangu yakikaa ndani yenu, ombeni lolote mtakalo nanyi mtatendewa.
Marko 11 : 25
25 Nanyi, kila msimamapo na kusali, sameheni, mkiwa na neno juu ya mtu; ili na Baba yenu aliye mbinguni awasamehe na ninyi makosa yenu. [
Yohana 16 : 24
24 Hata sasa hamjaomba neno kwa jina langu; ombeni, nanyi mtapata; furaha yenu iwe timilifu.
Luka 11 : 13
13 Basi, ikiwa ninyi mlio waovu mnajua kuwapa watoto wenu zawadi nzuri, je! Baba aliye mbinguni hatazidi sana kuwapa Roho Mtakatifu hao wamwombao?
Leave a Reply