Biblia inasema nini kuhusu Iconoclasm – Mistari yote ya Biblia kuhusu Iconoclasm

Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Iconoclasm

Kutoka 23 : 24
24 ⑤ Usiisujudie miungu yao, wala kuitumikia; wala usitende mfano wa matendo yao; bali utaiangamiza kabisa, na nguzo zao utazivunja vipande vipande.

Kutoka 34 : 13
13 ⑮ Bali utabomoa madhabahu zao, na kuvunjavunja nguzo zao, na kuyakatakata maashera[37] yao.

Hesabu 33 : 52
52 ⑩ ndipo mtakapowafukuza wenyeji wote wa hiyo nchi mbele yenu, nanyi mtayaharibu mawe yao yote yenye kuchorwa sanamu, na kuziharibu sanamu zao zote za kusubu, kuvunjavunja mahali pao pote palipoinuka;

Kumbukumbu la Torati 7 : 5
5 Lakini watendeni hivi; zivunjeni madhabahu zao zibomoeni nguzo zao, yakateni maashera yao, ziteketezeni kwa moto sanamu zao za kuchonga.

Kumbukumbu la Torati 7 : 26
26 ⑦ na usitie kitu kilicho haramu ndani ya nyumba yako, usije ukalaaniwa kama haramu hiyo; ukichukie kabisa na kukikataa kabisa, kwa kuwa ni kitu kilicholaaniwa.

Kumbukumbu la Torati 12 : 4
4 Wala msimfanyie hivyo BWANA, Mungu wenu.

Waamuzi 2 : 2
2 ④ nanyi msifanye agano lolote na hawa wenyeji wa nchi hii; yabomoeni madhabahu yao; lakini hamkuisikia sauti yangu; je! Mmefanya haya kwa sababu gani?

Yeremia 50 : 2
2 ⑦ Tangazeni katika mataifa, Mkahubiri na kutweka bendera; Hubirini, msifiche, semeni, Babeli umetwaliwa! Beli amefedheheka; Merodaki amefadhaika; Sanamu zake zimeaibishwa, Vinyago vyake vimefadhaika.

Mwanzo 35 : 4
4 ⑥ Nao wakampa Yakobo miungu migeni yote iliyokuwa mikononi mwao, na vipuli vilivyokuwa masikioni mwao, naye Yakobo akazificha chini ya mwaloni ulioko Shekemu.

Kutoka 32 : 20
20 Akaitwaa ile ndama waliyoifanya, akaichoma moto, akaisaga hata ikawa mavumbi, akainyunyiza juu ya maji, akawanywesha wana wa Israeli.

Waamuzi 6 : 32
32 Basi Yoashi akamwita Gideoni, Yerubaali siku hiyo, akisema, Baali na atete naye kwa ajili ya nafsi yake, kwa sababu ameibomoa madhabahu yake.

2 Samweli 5 : 21
21 Nao wakaziacha sanamu zao huko, na Daudi na watu wake wakaziondolea mbali.

1 Mambo ya Nyakati 14 : 12
12 Nao wakaiacha miungu yao huko; naye Daudi akaamuru, ikateketezwa kwa moto.

2 Wafalme 10 : 28
28 Ndivyo Yehu alivyomharibu Baali katika Israeli.

2 Wafalme 11 : 18
18 Watu wote wa nchi wakaiendea nyumba ya Baali, wakaiangusha; madhabahu zake na sanamu zake wakazivunjavunja kabisa, na Matani kuhani wa Baali wakamwua mbele ya madhabahu. Na Yehoyada kuhani akaweka walinzi wa nyumba ya BWANA.

2 Wafalme 18 : 6
6 Maana alishikamana na BWANA, hakuacha kumfuata, bali alizishika amri zake BWANA alizomwamuru Musa.

2 Wafalme 23 : 20
20 Akawaua na makuhani wote wa mahali pa juu waliokuwako huko, juu ya madhabahu, akateketeza mifupa ya watu juu yake; kisha akarejea Yerusalemu.

2 Mambo ya Nyakati 14 : 5
5 Tena akaondoa kutoka miji yote ya Yuda mahali pa juu na sanamu za jua; ufalme ukastarehe mbele yake.

2 Mambo ya Nyakati 15 : 16
16 Hata na Maaka mamaye Asa, mfalme akamwondolea cheo chake asiwe malkia, kwa kuwa amefanya sanamu ya kuchukiza kwa Ashera; basi Asa akaikata sanamu yake, akaiponda, akaiteketeza penye kijito cha Kidroni.

2 Mambo ya Nyakati 17 : 6
6 ⑦ Ukainuliwa moyo wake katika njia za BWANA; na zaidi ya hayo akapaondoa mahali pa juu, na Maashera, katika Yuda.

2 Mambo ya Nyakati 19 : 3
3 Walakini, yameonekana kiasi cha mema ndani yako, kwa kuwa umeyaondoa Maashera katika nchi, na moyo wako umeukaza kumtafuta Mungu.

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *