Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Hur
Kutoka 17 : 10
10 Basi Yoshua akafanya kama Musa alivyomwambia, akapigana na Amaleki; na Musa na Haruni na Huri wakapanda juu ya kile kilima.
Kutoka 17 : 12
12 Lakini mikono ya Musa ililegea; basi wakatwaa jiwe, wakaliweka chini yake akalikalia. Haruni na Huri wakaitengemaza mikono yake, mmoja upande huu na mmoja upande huu; mikono yake ikathibitika hata jua lilipokuchwa.
Kutoka 24 : 14
14 Akawaambia hao wazee, Tungojeeni hapa, mpaka tutakaporudi kwenu; na tazameni, Haruni na Huri wapo pamoja nanyi; kila mtu aliye na jambo na awaendee.
Kutoka 31 : 2
2 Angalia, nimemwita kwa jina lake Bezaleli mwana wa Uri, mwana wa Huri, wa kabila la Yuda;
Kutoka 35 : 30
30 ⑦ Kisha Musa akawaambia wana wa Israeli, Angalieni, BWANA amemwita kwa jina lake Bezaleli mwana wa Uri, mwana wa Huri, wa kabila la Yuda;
Kutoka 38 : 22
22 Na Bezaleli mwana wa Uri, mwana wa Huri, wa kabila la Yuda, akafanya yote BWANA aliyomwagiza Musa.
1 Mambo ya Nyakati 2 : 20
20 ⑮ Naye Huri akamzaa Uri; na Uri akamzaa Besaleli.
2 Mambo ya Nyakati 1 : 5
5 Tena madhabahu ya shaba, aliyoifanya Bezaleli mwana wa Uri, mwana wa Huri, ilikuwako huko mbele ya maskani ya BWANA; Sulemani na kusanyiko wakaiendea.
Hesabu 31 : 8
8 Nao wafalme wa Midiani wakawaua pamoja na watu wengine waliouawa; Evi, na Rekemu, na Suri, na Huri, na Reba, hao wafalme watano wa Midiani; Balaamu mwana wa Beori naye wakamwua kwa upanga.
Yoshua 13 : 21
21 ② na miji yote ya nchi tambarare, na ufalme wote wa Sihoni mfalme wa Waamori, aliyekuwa akitawala katika Heshboni, aliyepigwa na Musa pamoja na hao wakubwa wa Midiani, nao ni Evi, na Rekemu, na Suri, na Huri, na Reba, hao watawala wa Sihoni, waliokuwa katika nchi hiyo.
1 Wafalme 4 : 8
8 Na haya ndiyo majina yao. Mwana wa Huri, mlimani mwa Efraimu.
1 Mambo ya Nyakati 2 : 50
50 Hao walikuwa wana wa Kalebu. Wana wa Huri, mzaliwa wa kwanza wa Efrata; Shobali, babaye Kiriath-Yearimu;
1 Mambo ya Nyakati 4 : 4
4 na Penueli, babaye Gedori, na Ezeri, babaye Husha. Hao ndio wana wa Huri, mzaliwa wa kwanza wa Efrata, babaye Bethlehemu.
1 Mambo ya Nyakati 4 : 1
1 Wana wa Yuda; Peresi, na Hesroni, na Karmi, na Huri, na Shobali.
Nehemia 3 : 9
9 Na baada yao Refaya, mwana wa Huri akajenga, mtawala[3] wa nusu ya Yerusalemu.
Leave a Reply