Biblia inasema nini kuhusu hotuba yetu – Mistari yote ya Biblia kuhusu hotuba yetu

Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia hotuba yetu

Waefeso 4 : 29
29 ⑮ Neno lolote lililo ovu lisitoke vinywani mwenu, bali lililo jema la kumfaa mwenye kuhitaji, ili liwape neema wanaosikia.

Mathayo 15 : 11
11 Sikilizeni, mfahamu; Sicho kiingiacho kinywani kimtiacho mtu unajisi; bali kitokacho kinywani ndicho kimtiacho mtu unajisi.

Wakolosai 4 : 6
6 ⑥ Maneno yenu yawe na neema siku zote, yakikolezwa chumvi, ili mpate kujua jinsi iwapasavyo kumjibu kila mtu.

Mithali 18 : 20 – 21
20 Tumbo la mtu litajazwa matunda ya kinywa chake; Atashiba mazao ya midomo yake.
21 Mauti na uzima huwa katika uwezo wa ulimi; Na wao waupendao watakula matunda yake.

Mithali 17 : 28
28 Hata mpumbavu akinyamaza, huhesabiwa hekima; Akifumba midomo yake, huhesabiwa ufahamu.

Mithali 15 : 4
4 Ulimi safi ni mti wa uzima; Bali ukorofi wa ulimi huvunja moyo.

Mithali 15 : 1 – 2
1 Jawabu la upole hugeuza hasira; Bali neno liumizalo huchochea ghadhabu.
2 Ulimi wa mwenye hekima hutamka maarifa vizuri; Bali vinywa vya wapumbavu humwaga upumbavu.

Mhubiri 5 : 2 – 4
2 Usiseme maneno ya ujinga kwa kinywa chako, wala moyo wako usiwe na haraka kunena mbele za Mungu; kwa maana, Mungu yuko mbinguni, na wewe upo chini, Kwa hiyo maneno yako na yawe machache.
3 Kwa maana ndoto huja kwa sababu ya shughuli nyingi; na sauti ya mpumbavu kwa njia ya wingi wa maneno.
4 Wewe ukimwekea Mungu nadhiri, usikawie kuiondoa; kwa kuwa yeye hawi radhi na wapumbavu; basi, uiondoe hiyo uliyoiweka nadhiri.

Yakobo 1 : 26
26 Mtu akidhani ya kuwa anayo dini, wala hauzuii ulimi wake kwa hatamu, ili hali akijidanganya moyo wake, dini yake mtu huyo haifai.

Mithali 10 : 31 – 32
31 Kinywa cha mwenye haki hutoa hekima; Bali ulimi wa ukaidi utakatiliwa mbali.
32 Midomo ya mwenye haki huyajua yatakayokubaliwa; Bali kinywa chao wasio haki hunena ukaidi.

Waefeso 5 : 4
4 wala aibu wala maneno ya upuzi wala ubishi; hayo hayapendezi; bali kuwepo kushukuru.

Mithali 16 : 24
24 Maneno yapendezayo ni kama sega la asali; Ni tamu nafsini, na afya mifupani.

Mithali 17 : 27
27 Azuiaye maneno yake ni mwenye maarifa; Na mwenye roho ya utulivu ana busara.

Mithali 12 : 25
25 ⑦ Uzito katika moyo wa mtu huuinamisha; Bali neno jema huufurahisha.

Mithali 21 : 23
23 Mtu azuiaye kinywa chake na ulimi wake, Atajilinda nafsi yake na taabu.

2 Timotheo 2 : 16
16 Jiepushe na maneno machafu yasiyo na maana, ambayo si ya dini; kwa kuwa wataendelea zaidi katika maovu,

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *