Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Heshima
Matendo 10 : 26
26 ⑤ Lakini Petro akamwinua, akasema, Simama, mimi nami ni mwanadamu.
Matendo 14 : 18
18 Na kwa maneno hayo wakawazuia watu kwa shida, wasiwatolee dhabihu.
Ufunuo 19 : 10
10 ⑳ Nami nikaanguka mbele ya miguu yake, ili nimsujudie; akaniambia, Angalia, usifanye hivi; mimi ni mtumishi mwenzako na wa ndugu zako walio na ushuhuda wa Yesu. Msujudie Mungu. Kwa maana ushuhuda wa Yesu ndio roho ya unabii.
1 Wafalme 1 : 16
16 Bathsheba akainama, akamsujudia mfalme. Naye mfalme akamwuliza, Wataka nini?
1 Wafalme 1 : 23
23 Wakamwambia mfalme wakasema, Tazama, Nathani, nabii. Naye alipoingia ndani mbele ya mfalme, akamsujudia kifudifudi.
1 Wafalme 1 : 31
31 Ndipo Bathsheba akainama kifudifudi, akamsujudia mfalme, akasema, Bwana wangu mfalme Daudi na aishi milele.
Esta 3 : 2
2 Nao watumishi wote wa mfalme, walioketi langoni pa mfalme, wakainama na kumsujudia Hamani, maana ndivyo mfalme alivyoamuru wamfanyie. Lakini Mordekai hakumwinamia, wala kumsujudia.
Esta 3 : 5
5 Hata Hamani alipoona ya kwamba Mordekai hamwinamii wala kumsujudia, alighadhibika sana.
Leave a Reply